.jpg)
Anasisitiza umuhimu wa kusimama imara katika kuchagua amani, kuheshimiana, na kutumia mifumo ya kisheria kueleza tofauti za kimitazamo zinazoweza kujitokeza.
Mtazamo huo unaungwa mkono na mkazi wa Dar es Salaam, Rehema Crispin, ambaye anaielezea amani kama kitu chenye thamani isiyopimika. Rehema anaamini kuwa amani ndiyo gundi inayowaunganisha Watanzania kuishi kwa upendo na ushirikiano, jambo linalotupa fahari kama taifa. Anatoa wito kwa kila mmoja wetu kuilinda na kuidumisha amani hiyo kwa gharama yoyote ili kuhakikisha maendeleo ya nchi hayakwami.
Kwa upande mwingine, Emmanuel Mapury kutoka mkoani Mwanza, anagusia uhusiano wa moja kwa moja kati ya amani na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Mapury anakumbusha kuwa maisha ya Mtanzania yanategemea uhuru wa kutoka kwenda kutafuta riziki ili apate kula. Anasititiza kuwa ili Mtanzania akafanye kazi na kupata kipato, ni lazima kuwepo na utulivu, hivyo kila mwananchi anapaswa kuwa balozi mzuri kwa kupinga vurugu za aina yoyote ile zinazoweza kuvuruga mnyororo wa uzalishaji na maisha ya kila siku.
Sauti hizi kutoka Songwe hadi Mwanza, na Dar es Salaam hadi mikoani, ni kielelezo tosha kuwa amani ni taji ambalo Watanzania wameamua kulivaa kwa pamoja ili kuvuka salama kuelekea mustakabali wa maendeleo ya kweli.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464