` SAUTI ZA MTAA: NJAA, HOFU NA MAISHA MAGUMU YANATAKA UMOJA IMARA WA KITAIFA

SAUTI ZA MTAA: NJAA, HOFU NA MAISHA MAGUMU YANATAKA UMOJA IMARA WA KITAIFA




Sauti za wananchi wa kawaida zimebainisha jinsi vurugu zilivyosimamisha maisha. Familia ziliteseka na njaa, watoto walikosa shule, na wazazi walishindwa kutekeleza majukumu yao ya uongozi.


Habib Sadick anaeleza, kama kiongozi wa familia: "Mimi ni kiongozi katika familia... nina mke na mtoto, siku tano ni nyingi sana hata kama wewe ni tajiri una fedha huwezi kuzifanyia chochote kwa kuwa kipindi kile hakina amani hata kidogo. Maisha tuliyopitia ni funzo."

Salma Juma Kimaro anaongeza athari kwa jamii: "Mzunguko wetu wa maisha utoke ndio upate ridhiki. Wengi tumeathirika, watoto shuleni walikuwa majumbani hakuna chakula."

Haya ni maumivu yanayotutaka tuimarishe Umoja wa Kitaifa na Mshikamano. Mzee wa Jadi Juma Mbagho anasema: "Katika mila zetu, tunafundishwa kuketi pamoja baada ya ghasia. Tusiache chuki ikajenga mizizi. Umoja wetu ndio ngao yetu kuu."

Mbagho anasisitiza kuwa Taifa linahitaji kuanzisha midahalo ya kijamii inayoongozwa na viongozi wa kijadi, dini, na serikali ili kujenga imani na kupunguza hofu iliyojengeka baada ya vurugu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464