` VIONGOZI WA DINI MKOA WA SHINYANGA WAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA OCTOBA 29

VIONGOZI WA DINI MKOA WA SHINYANGA WAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA OCTOBA 29

  

Kamati ya maridhiano ya Mkoa wa Shinyanga inayoundwa na Viongozi wa Dini, Machifu, Viongozi wa Serikali na

wawakilishi wa Wananchi wa Mkoani Shinyanga wameiasa jamii kujitokeza kupiga kura ifikapo octoba 29 mwaka huu ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi bora ambao watawaletea maendeleo kuanzia ngazi ya mitaa.

 

Viongozi hao Kwa umoja wao wamezimia kuiunga serikali mkono katika kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura kwa amani na utulivu.

 

Viongozi hao wameyasema hayo katika kikao maalum cha kujadili namna ya kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa tarehe 29 mwezi huu wa Oktoba 2025 Kikao ambacho kimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita na mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Zamani wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.

 

Chifu Kidiola wa Pili ambaye ni mwenyekiti wa Machifu wa Mkoa wa Shinyanga amesema machifu wako tayari kutumia mbinu zao za uongozi kuhakikisha wananchi katika maeneo yao wanajitiokeza kupiga jura na kutekeleza maelekezo ya serikali.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Mboni Mhita akizungumza na wajumbe wa Kamati ya maridhiano ya Mkoa wa Shinyanga.

Aliyekuwa waziri wa maliyasili na utalii LAZARO NYALANDU ameendelea kuwasihi viongozi wa dini,machifu na wazee kuliombea taifa hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na kuwataka wananchi kujitokeza siku nya tarehe 29 mwezi huuwa Oktoba 2025 kupiga kura na kasha kuwenda kuendelea na shughuli zao za maiosha wakati wakisubiri matokeo yatangazwe.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga MBONI MHITA amewahakikisha wananchi wa Mkoa huo Amani na utulivu siku ya kupiga kura na kuwa Mkoa itakuwa salama wasiogope kujitiokeza kwakuwa serikali kupitia vyombo nvya usalama iko tayari kuwalinda wananchi wake.


Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Shinyanga ,Chifu Kidola wa Pili.












Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464