` KAZI NA UTU: AMANI NA UTULIVU NDIO MSINGI WA SAYANSI!

KAZI NA UTU: AMANI NA UTULIVU NDIO MSINGI WA SAYANSI!


Serikali Ya Awamu Ya Sita Yaweka Msingi Imara Kwa Wasichana


Tukiwa tunaelekea katika Uchaguzi, ni muhimu kutambua kwamba maendeleo ya taifa letu yanategemea amani na utulivu. Taifa linahitaji vijana wanaojua Sayansi, na hii inawezekana tu katika mazingira ya utulivu, ambapo masomo yanaendelea vizuri.


Serikali ya Awamu ya Sita imejitosa kikamilifu kuhakikisha watoto wa kike wanachomoza katika masomo ya Sayansi kwa vitendo. Utekelezaji wa ujenzi wa Shule 26 za Sekondari za Wasichana za Sayansi (Shule moja kwa kila Mkoa wa Tanzania Bara) ni ushahidi wa azma hii.


Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga ni mfano mmoja wa shule hizi ambazo zimejengwa mahususi kwa lengo la kuwawezesha watoto wa kike kufundishwa Sayansi kwa ubora, na hivyo kuongeza idadi ya Wanasayansi nchini.


Jumla ya Shilingi 155,240,120,476.81 zimetumika katika miradi hii ya maendeleo ya elimu.


Ubora wa shule hizi unazdhirisha  na utimilifu wake kama wanafunzi hawa wanavyotumia maabara za kisasa (kwenye picha). Lakini maendeleo haya yataendelea na kuwa na maana kama tu tukiilinda amani.


Mwanafunzi Mmoja Aliyefaidika wa shule ya Shinyanga alisema:"Ninamshukuru sana Rais wetu kwa kuwajali wasichana. Miradi hii imetusaidia sana kwa kutuondolea vishawishi na kutupatia mazingira bora ya kupata elimu bora. Tumeona kwamba wasichana tukipewa nafasi, tunaweza kufanya makubwa katika Sayansi kama watoto wa kiume!"


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464