` JACKLINE ISARO:SITAKUWA KIONGOZI WA KUKAA OFISINI KILA BAADA YA MIEZI MITATU NITAKUWA NAFANYA MIKUTANO YA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

JACKLINE ISARO:SITAKUWA KIONGOZI WA KUKAA OFISINI KILA BAADA YA MIEZI MITATU NITAKUWA NAFANYA MIKUTANO YA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGOMBEA Udiwani Kata ya Ngokolo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Jackline Isaro,amewahidi wananchi wa Kata hiyo,kwamba wakimpatia ridhaa ya kuwa diwani wao,hata kuwa kiongozi wa kukaa ofisini,na kila baada ya miezi mitatu atakuwa akifanya mikutano ya hadhara,kwa kila mtaa kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.

Amebainisha hayo leo Oktoba 16,2025 kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika Mtaa wa Mwinamila Kata ya Ngokolo.
Amesema,kiongozi yeyote anayependa kukaa Ofisini hawezi kuleta maendeleo,hivyo yeye takuwa wa tofauti kwa kuzunguka kila mtaa kusikiliza changamoto ambazo zinawakabili wananchi wake na kuzipatia ufumbuzi.

“Mkinipatia ridhaa ya kuwa diwani wenu Oktoba 29,sitakuwa kiongozi wa kukaa ndani,nitashirikiana na viongozi wa serikali za mtaa kufanya mikutano ya hadhara kila baada ya miezi mitatu kusikiliza kero zenu na kuzipatia ufumbuzi,”amesema Jackline.
Ametoa wito pia kwa wananchi,kwamba wakiitwa kwenye mkitano hiyo wajitokeze kwa wingi, ili kusema changamoto zao na kutatuliwa.

Amesema changamoto ambazo zinawakabili wafanya biashara wa soko la mitumbani atazifanyia kazi,huku akiwahidi pia wanawake,vijana kwamba atawapigania kwenye suala la mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri ili wapate kunufaika nayo na kuinuka kiuchumi.
Aidha,amewaomba pia wananchi kwamba siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kuwachagua wagombea wote wanaotokana na CCM,na kwamba wasikubali kushawishiwa kufanya maandamano yasiyo na tija ambayo yatavuruga amani ya nchi.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe,amewaomba wananchi wa Ngokolo waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi,na kuwapatia ridhaa ya miaka mitano tena kuongoza,ili waendelee kuwaletea maendeleo, sababu ni chana chenye sera na ilani nzuri inayogusa maslahi ya wananchi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni Ngokolo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe (kulia)akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM,Mgombea Udiwani Kata ya Ngokolo Jackline Isaro.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe (kulia)akimnadi na kumuombea kura Mgombea Udiwani Kata ya Ngokolo Jackline Isaro,pamoja na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi na Mgombea Urais,Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akitoa elimu namna ya kupiga kura siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29.
Mgombea Udiwani Kata ya Ngokolo Jackline Isaro akimwaga sera kwa wananchi huku akiwa ameshika Ilani ya CCM.
Diwani Mteule wa Vitimaalum Tarafa ya Mjini kutoka Kata ya Ngokolo Veronica Masawe akiwanga sera kwa wananchi.
Mgombea Udiwani Kata ya Ngokolo Jackline Isaro akipiga Magoti kuomba kura kwa wananchi.
Kura zikiendelea kuombwa kwa wananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464