Salum Mwalimu: Ninaidai CHADEMA mamilioni

KATIBU Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu amejibu maswali ya baadhi ya watu wanaohoji wapi chama hicho kinatoa fedha za kujiendeshea katika ziara zake hizo kinazoendelea nazo.
Mwalimu amesema wakiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), walikuwa wanatoa fedha zao kuchangia shughuli mbalimbali na kwamba njia hiyo hiyo ndio wanaitumia kukiendesha CHAUMMA.
Aliwashangaa baadhi ya watu wanaodai kwamba njaa zao ndizo zimewahamisha chama cha cha zamani kwenda huko waliko sasa. "Baadhi ya watu wanasema tumehama kwa sababu ya njaa, waulizeni ninawadai kiasi gani, ninakidai chama(CHADEMA) mamilioni ya shilingi.
"Sijawahi kuwa mbunge, sijawahi kuwa diwani, nilikuwa nazitoa za kwangu, za wazazi wangu, za watoto wangu ninakikopesha chama ili tujenge chama, eti leo ninaambiwa nina njaa,"aliuliza. Alidai kwamba fedha anazokidai CHADEMA siyo ndogo ni nyingi.
SOMA ZAIDI CHANZO NIPASHE.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464