` DIWANI NDETTOSON AELEZA NAMNA KISHAPU INAVYOIMARIKA KILA SEKTA

DIWANI NDETTOSON AELEZA NAMNA KISHAPU INAVYOIMARIKA KILA SEKTA

 

Diwani wa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akizungumza baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata kipindi cha Januari-Juni 2025 kwenye mkutano mkuu wa Chama ngazi ya Kata Juni 9,2025 katika ukumbi wa mikutano wa chama hicho Wilaya

Na Sumai Salum-Kishapu

Diwani wa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson Juni 9,2025 ameendelea kuonyesha usimamizi mzuri ulioleta mabadiliko wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2025 Kata ya Kishapu mbele ya wananchi, viongozi wa CCM Kata na Wilaya, wajumbe wa kamati ya maendeleo ya Kata, na wageni waalikwa katika ukumbi wa mikutano wa Ccm Wilaya.


Katika taarifa hiyo iliyosheheni mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo, Mhe. Ndettoson amegusia maeneo kadhaa muhimu yakiwemo ulinzi na usalama, elimu, afya, maendeleo ya jamii,maji, kilimo na mifugo, mazingira, pamoja na huduma za Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).

Mhe. Ndettoson ameeleza kuwa sekta ya elimu imeendelea kuimarika kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na ongezeko la waalimu wa masomo mbalimbali Kata ikiwa na jumla ya shule 9( Msingi 7 na Sekondari 2)

Katika sekta ya afya ameongeza hali ya utoaji wa huduma umeimarika katika hospitali Dr.Jakata Mrisho Kikwete,Kituo cha afya Kishapu na Zahanati ya Lubaga kwa kuwahudumia wagonjwa wa ndani na nje huku wengine wakitoka Mkoa wa Simiyu pamoja na kununua vifaa tiba na dawa kwa mapato ya ndani na serikali kuu, ingawa bado kuna uhitaji wa watumishi 126 katika kada mbalimbali za afya ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Amebainisha kuwa jitihada za Serikali ya awamu ya sita kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu zimechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa huduma ya maji safi na salama, huku sekta ya kilimo na mifugo ikiendelea kupokea usaidizi kupitia pembejeo za ruzuku wametoa mafunzo kwa wakulima 257 kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo bora na huduma za ugani.

Kuhusu ulinzi na usalama, Mhe. Ndettoson amesema kuwa hali ni shwari na kwamba jamii imeendelea kushirikiana na vyombo vya dola kudumisha amani huku utoaji taarifa wa uhalifu na wahalifu umeongezeka hivyo matukio mbalimbali yanayohatarisha usalama yapo yaliyodhibitiwa kabla ya utekelezwaji wake na elimu bado inaendelewa kutolewa.

Kuhusu Afya na Mazingira pia yamepewa kipaumbele kwa kampeni za usafi wa Kata yote ambazo zimeongeza uelewa na ushiriki wa wananchi hivyo kupelekea maeneo ya makazi na hata biashara,viwanda pamoja na machinjio kuzingatia kanuni na taratibu za afya.

"Ni kweli tunao ukosefu wa gari la maji taka na taka ngumu lakini mwaka wa fedha ujao mambo yatakuwa sawa kwa sababu uko mpango kabambe wa Halmashauri kuwanufaisha wananchi wa Kishapu kwa kuwasogezea huduma hiyo", amesema Diwani huyo.

Ameongeza kuwa Tarura imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara za ndani ya Kata ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao na shughuli zingine za wananchi.

Amempongeza Diwani wa viti maalum Kata hiyo Mhe.Felister Yahula,wananchi,viongozi wa Chama,watendaji na wataalamu wa Kata na serikali ya awamu ya sita kwa ushirikiano alipopata kipindi cha usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.

Baadhi ya wajumbe na wageni waalikwa wakizungumza na Malunde 1 blog kujua mapokeo yao ya taarifa wametoa pongezi kwa kusimamia kwa weledi utekelezaji wa miradi ya maendeleo, wakisema kuwa anatoa mfano bora wa kiongozi anayesimamia Ilani ya Chama chake kwa vitendo huku wakiiomba serikali kuongeza juhudi kuendelea kupunguza uhaba wa wahudumu wa afya na kuendelea kuboresha miundombinu katika sekita ya elimu na barabara.Diwani wa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson (kulia) na Diwani wa viti maalumu wa Kata hiyo Mhe.Felister Yahula wakitoa pongezi kwa ushirikiano walioupata kipindi cha miaka 5 ya uongozi wao katika kusimamia miradi mbalimbali ya Kata kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi Juni 9,2025 kipindi cha Januari-Juni 2025Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Cornel LugodaKaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Neema Godwin akijibu maswali ya wajumbe wa mkutano wa usomaji taarifa wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya kishapu Juni,9,2015Afisa afya Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Kenneth Mauki akizungumza kwenye mkutano huo wa uwasilishaji taarifa ya Kata kutekelza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Juni,9,2015 kwa kipindi cha Januari-Juni 2025Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Igaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga na mgeni mwalikwa wa mkutano huo Makolo J.Makolo akizungumzia utekelezaji wa ilani ya Chama hicho kwa Kata ya Kishapu kwa kipindi cha Januari-Juni 2025 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464