` MADIWANI KISHAPU WAPITISHA MIPANGO NA BAJETI YA FEDHA ZA CSR BILIONI 1 KUTOKA MGODI WA MWADUI

MADIWANI KISHAPU WAPITISHA MIPANGO NA BAJETI YA FEDHA ZA CSR BILIONI 1 KUTOKA MGODI WA MWADUI

MADIWANI KISHAPU WAPITISHA MIPANGO NA BAJETI YA FEDHA ZA CSR BILIONI 1 KUTOKA MGODI WA MWADUI

Na Marco Maduhu,KISHAPU

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu,wamepitisha mipango na bajeti ya fedha za CSR Sh.bilioni 1 zilizotolewa na Mgodi wa Almasi Mwadui, kupitia mpango wa Uwajibikaji wa Makampuni kwa Jamii (CSR) kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Wamepitisha mipango hiyo leo Juni 13,2025 katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kwa kilichoitishwa mahsusi kujadili na kupitisha matumizi ya fedha hizo.

Afisa Mipango na Mtaribu wa fedha za CSR kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu James Zitto,awali akiwasilisha taarifa ya fedha ya mipango na bajeti ya fedha hizo,amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 Mgodi wa Almasi Mwadui umetoa sh.bilioni 1 kwa ajili utekelezaji wa miradi.
“Asilimia 40 ya fedha hizi zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo yanayozunguka mgodi, na asilimia 60 zitatumika kwa miradi ya kimkakati ya halmashauri,” amesema Zitto.

Baada ya mjadala wa kina kutoka kwa madiwani, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri aliuliza iwapo wanaridhia kuipitisha bajeti hiyo, ambapo kwa kauli moja madiwani waliidhinisha rasmi bajeti hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Emmanuel Johnson, amewasihi madiwani kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa uadilifu mkubwa na kuepuka migogoro inayoweza kusababisha mgodi kusitisha utoaji wa fedha hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu,Peter Masindi, aliwahimiza madiwani na viongozi wengine kutowaingilia wakandarasi wanaotekeleza miradi, wala kuwaomba "kitu kidogo", akisisitiza kuwa tamaa binafsi zisije kuchafua sifa zao au kuharibu utekelezaji wa miradi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Mkurugenzi wa Kishapu Emmanuel Johnson akizungumza.
Afisa Mipango na Mtaribu wa fedha za CSR kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu James Zitto,akiwasilisha fedha za CSR.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Francis Manyanda akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464