Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Aliyekuwa diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu,amechukua fomu ya kutetea kiti chake cha Udiwani katika Kata hiyo,ambayo aliitumika ndani ya miaka mitano.
Amechukua fomu hiyo leo Juni 29,2025 katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Ngokolo, na kukabidhiwa na Kaimu Katibu Kata ya Ngokolo (CCM) Jafari Juma.
Akizungumza mara baada ya kuchukua Fomu hiyo,amesema akishapewa ridhaa na Chama kwa mara nyingine tena kupeperusha Bendera kwenye uchaguzi Mkuu 2025, atazungumza mambo mengi ambayo ameyafanya ya kuwaletea maendeleo wananchi tangu aliposhika nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu 2020.

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu (kushoto)akikabidhiwa Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama Kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu 2025, na Kaimu Katibu Kata ya Ngokolo CCM Jafari Juma.
Victor Mkwizu awali akiingia na usafiri wa Boda Boda kwenye Ofisi za CCM Kata ya Ngokolo kuchuka Fomu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464