WANNE WACHOMWA MOTO KAHAMA:
NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amethibitisha tukio la kusikitisha lililotokea alfajiri ya leo Juni 17, 2025, katika Mtaa wa Mhongolo, Manispaa ya Kahama, ambapo watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni vibaka wameuawa kwa kupigwa mawe na kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.
Kamanda Magomi amelaani vikali tukio hilo na kusisitiza kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kujichukulia sheria mkononi, akibainisha kuwa uchunguzi mkali umeanza huku msako wa kuwatafuta waliohusika ukiendelea.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Ibrahimu Jacob, mkazi wa Mhongolo amesema eneo hilo limegeuka kuwa hatari hasa nyakati za usiku ambapo watu huvamiwa na kuporwa mali zao.
Ibrahimu amesema yeye mwenyewe ameshawahi kupigwa na kuporwa zaidi ya mara moja ambapo ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kingdom doria na kusisitiza kuwa baadhi ya vibaka hujificha kwenye maeneo ya miembe karibu na shule.
SOMA ZAIDI CHANZO UHESO
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464