` NAIBU WAZIRI KHAMIS ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

NAIBU WAZIRI KHAMIS ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

NAIBU WAZIRI KHAMIS ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Khamis, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kutunza mazingira,ili kukabiliana na changamoto ya kuenea kwa hali ya jangwa na ukame nchini.
Ametoa wito huo leo Juni 17,2025 wakati akitoa hotuba kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani,maadhimisho ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Shinyanga.

Amesema ni jikumu la kila Mtanzania, kuyatunza mazingira ili kukabiliana na hali ya jangwa na ukame katika kulinda mazingira kwa mustakabali wa taifa.
“Wananchi waongeze jitihada za kupanda miti hasa ile inayostahimili ukame, waache kukata miti hovyo na kuchoma mkaa kwa ajili ya kupikia. Tunawasihi watumie nishati safi ili kuokoa mazingira yetu,” amesema Khamis.

Aidha, amewataka wakulima, wafugaji na wachimbaji wa madini kuhakikisha kuwa shughuli zao haziwi chanzo cha uharibifu wa mazingira, ikiwamo ukataji miti usiozingatia sheria na taratibu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, amewaonya wananchi wa mkoa huo dhidi ya ukataji miti ovyo, akisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuharibu mazingira.

“bado kuna wananchi wanaendelea kukata miti hivyo sheria zipo wazi, hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakaye bainika kuharibu mazingira,” amesema Mtatiro.
Aidha,amesema katika mkoa huo kuna kampeni ambazo zinaendelea na utunzaji wa mazingira pamoja na kupanda miti, na kwamba Shinyanga ya sasa siyo ile ya zamani ambayo ilikuwa haina miti kabisa, lakini sasa hivi kuna uhafadhari ambapo miti mingi imepandwa.

Kauli Mbiu ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya ukame duniani mwaka huu 2025 inasema “Ongoa Ardhi,kufungua fursa.

TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Khamis akizungumza.
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Khamis akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Khamis akipanda mti katika Kituo cha Afya Kambarage.
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Khamis akipanda mti katika Kituo cha Afya Kambarage.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akipanda mti katika Kituo cha Afya Kambarage.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akipanda mti katika Kituo cha Afya Kambarage.
Viongozi wa dini wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro wakipanda mti.
Maadhimisho yakiendelea.
Picha za pamoja zikipigwa.
Matembezi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464