` KISHAPU IMEPATA HATI SAFI

KISHAPU IMEPATA HATI SAFI

KISHAPU IMEPATA HATI SAFI

Na Marco Maduhu,KISHAPU

HALMASHAURI ya wilaya ya Kishapu imepata Hati Safi,katika mwaka wa fedha 2023/2024 unaoishia juni 30 2024,huku Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johson,akiahidi hoja 33 ambazo zipo kwenye utekelezaji zitafanyiwa kazi haraka ili zipate kufungwa.
Katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2023/2024 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. alibua hoja 38,ambapo hoja 5 zimehakikiwa na kufungwa zikiwapo mbili za zamani,kubaki hoja 33 ambazo zimepo kwenye utekelezaji, na kwamba kufuatia ukaguzi huo wa fedha za umma,Halmashauri ya Kishapu imepata Hati Safi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson,akizungumza kwenye kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani la Halmashauri hiyo leo Juni 13,2025,cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 unaoishia juni 30,2024,amesema kwamba hoja 33 ambazo zipo kwenye utekelezaji zitashughulikiwa kwa wakati na kufungwa.
“Katika Hoja hizi 33 ambazo zipo kwenye utekelezaji, tutajitahidi kila kiambata kipelekewe kwa wakati ili hoja hizo zipate kufungwa,na tunampongeza pia Rais Samia Suluhu Hassan,sababu zile hoja za kisera nyingi zimeshajibiwa ikiwamo kuajiri Watumishi,”amesema Johnson.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Francis Manyanda,amewaagiza Wakuu wa Idara,kuwa kila mmoja aanze kutafuta viambata ili kujibu hoja hizo na zifungwe, na kwamba katika Baraza lijalo mara baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wasikute hoja hizo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana,ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata Hati Safi,huku akisisitiza hoja za miradi viporo waiwekee kipaumbele ili waikamilishe.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,ameelekeza kwamba maelekezo yote ambayo yametolewa na CAG kwamba yafanyiwe kazi,ili kutoendelea kuwepo kwa hoja hizo.

Aidha,ameipongeza Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za umma,pamoja na ukusanyaji wa mapato na kwamba Kishapu ya miaka 2020, siyo ya sasa ambapo imepiga hatua kubwa kimaendeleo,huku akisisitiza kasi ya ukusanyaji mapato iongezeke, na yakusanywe kwa uaminifu.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Francis Manyanda akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza.
Mkazi wa Nje CPA Yusuph Mabwe akizungumza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson akizungumza.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana akizungumza.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464