HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA KUANZA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA MATIBABU YA MACHO
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imeanzisha rasmi huduma za matibabu ya kibingwa ya macho,huduma ambayo itaanza Rasmi kutolewa June 2 mwaka huu.
Dk.John Luzila.
Hayo yamebainishwa leo Mei 30,2025 na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo Dk.John Luzila,wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema siku ya uzinduzi wa huduma hiyo,itaambatana na “Camp ya utoaji wa matibabu ya macho kwa wananchi kuanzia June 2 hadi 6, na baada ya hapo huduma zitaendelea kama kawaida na itakuwa ikitolewa mara mbili kwa wiki hospitalini hapo.
“Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga tuna anzisha rasmi utoaji wa huduma za kibingwa za macho,ambapo tuna anza rasmi June 2 mwaka huu,”amesema Dk.Luzila.
Amesema kwamba wana daktari Bingwa wa Macho, amabye walimpeleka masomo, pamoja na kununua vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya utoaji wa huduma hizo vyenye thamani ya sh.milioni 79.
“Huduma ambazo zitakuwa zikitolewa kwenye Kliniki ya kibingwa ya macho, ni uchunguzi wa kina wa macho,mtoto wa jicho,presha ya macho, na Arrege ya macho,”amesema Dk.Luzila.
Nao baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwamo Yohana Shija, ameshukuru kwa kuanzishwa kwa huduma hiyo ya matibabu ya kibingwa ya macho katika hospitali hiyo, kwamba itawarahishia kupata huduma karibu na maeneo yao.
Naye Janeth Kalikale,amesema kwamba huduma hizo zitawaepusha na gharama kubwa ya kufuata matibabu hayo,katika hospitali kubwa ikiwamo Bugando na Mhimbili sababu ya kufuata madaktari bingwa,lakini sasa hivi huduma zote watapata hapo hapo Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464