Ujumbe wa 'SCAN CODE TO APPLY' ya Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga watua Shule ya Sekondari Bama iliyopo Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Ujumbe huo umefikishwa na Afisa Habari wa Chuo Cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga Josephine Charles katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Shule za Sekondari Mkoani Manyara kwa lengo la kutoa Elimu ya namna ya kujiunga na chuo hicho,kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kusoma fani za Afya na kuwatangazia wanafunzi mikopo inayotolewa na Serikali kwa kozi za Radiology, Physiotherapy na Medical Laboratory ili waweze kusoma kwa malengo.
Aidha Chuo hicho kinafundisha kozi 8, Sita zikiwa niza Afya na mbili zikiwa za Ufundi ambazo ni Clinical medicine, Nursing & Midwifery, Pharmaceutical Sciences, Medical Laboratory, Physiotherapy na Radiology, pia kozi za Ufundi ni Laboratory Assistant na Computer.
Hata hivyo wanafunzi wote wenye vigezo vya kusoma fani za Afya na Ufundi wametakiwa kutuma maombi ya kujiunga na chuo sasa hivi kwa njia ya ku Scan Code kupitia QR Code, kupitia tovuti ya Chuo www.kchs.ac.tz , kufika Chuoni Kolandoto Shinyanga au kupiga simu namba 0742155623.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464