` UWT WILAYA YA SHINYANGA MJINI WAMEANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA KATA KWA KATA

UWT WILAYA YA SHINYANGA MJINI WAMEANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA KATA KWA KATA



Na Mwandishi wetu,SHINYANGA

Viongozi wa umoja wa wanawake wa Tanzania U.W.T ( CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wameanza ziara kwenye kata zote,inayolenga kuimarisha uhai wa wanachama wake.

Katika siku ya kwanza ya ziara yao,viongozi hao wa U.W.T wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi Rehema Nhamanilo wamezungumza na wanachama wa jumuiya hiyo katika kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga ambapo wamehamasisha zaidi kuhusu uhai wa wanachama na jumuiya zake, na kulipa ada kama inavyoelekezwa.

Akizungumza katika mkutano uliojumuisha viongozi ngazi ya kata na matawii,pamoja na wenyeviti na wajumbe wa mitaa,vijiji na vitongoji wa kata hiyo, mwenyekiti wa U.W.T wilaya ya Shinyanga mjini Bi Rehema Nhamanilo amewataka kuendeleza umoja na mshikamano,kuwajibikia majukumu yao kwa weredi,ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya kikanuni, ili kukiimarisha chama na jumuiya zake

Mama Nhamanilo ameonya viongozi hao kuepuka makundi yasiyokuwa na tija hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais,wabunge na madiwani,kwa kuwa yanaweza kusababisha mpasuko ndani ya chama.

Mwenyekiti huyo amesisitiza viongozi hao kuwa chachu ya umoja na mshikamano zaidi miongoni mwao na kuepuka makundi yasiyokuwa na tija.

Amewakumbusha kuendelea kuwapa ushirikiano wabunge na madiwani waliopo madarakani,ili kuwatia moyo waweze kukamilisha majuku yaliyo mbele yao.

kwa upande wake katibu wa U.W.T ( CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi amesisitiza zaidi kuhusu uhai wa jumuiya hiyo na,ambapo amehamasisha kusimamia ulipaji wa ada,na kusajili wanachama wapya.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464