Header Ads Widget

CRDB BENKI KUFANIKISHA MALENGO YA WAFANYABIASHARA -SHINYANGA.

 CRDB BENKI KUFANIKISHA MALENGO YA WAFANYABIASHARA -SHINYANGA.Na Shaban Alley.

Benki ya CRDB kuendelea kuimarisha mahusiano na wateja wake wa muda mrefu mkoani wa Shinyanga ili kuwapa fursa mbalimbali za benki katika kufanikisha malengo ya wafanyabiashara hao.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela wakati akiwa katika ziara ya kutembelea wateja wa benki hiyo mkoani Shinyanga ndani ya wiki hii.NSekela amewahakishia wateja hao kuwa benki itaendelea kuimarisha  huduma na bidhaa za benki ili wafanikisha malengo ya wafanyabiashara.

Nsekela amekutana na wafanyabiashara makundi mbalimbali ndani ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara. Miongoni mwa wateja waliotembelewa na benki ya CRDB ni Bw, Jackton Koyi mmiliki wa shule za KOM mkoani shinyanga.

KOM –class ni moja ya wateja wetu wa muda mrefu ambaye kampuni yake inajishughulisha na uuzaji, utengenezaji, usambazaji vifaa vyote vinavyohusiana na kompyuta huku pia wamiliki kituo cha mafunzo ya kompyuta mjini shinyanga “anasema Nsekela

Niendele kukaribisha wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo kufika katika matawi yetu kwani tuna bidhaa na huduma zinazolenga mahitaji ya makundi mbalimbali ya Wafanyabiashara. Anasema Nsekela.

Mkurugenzi Mtendajiw a CRDB benki,w. Abdulmajid Nsekela akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa KOM-Class Limited,Bw.Jacton Koyi

CRDB benki imekuwa katika wakati mzuri wa kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea mazingira salama ya kibiashara kwa kuendelea kutumia bidhaa na huduma za benki hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa KOM –Class Limited,Bw.Jackton Koyi  ambaye anamiliki shule ya msingi na sekondari ya KOM, ameeleza kuwa benki hiyo ilikuwa ni msaada kwake katika uwekezaji alioanza toka  mwaka 2006 kwa mradi wa shule ya sekondari na kufanikisha  wahitimu elfu ishirini na moja(21,000)

Post a Comment

0 Comments