Header Ads Widget

MADIWANI WILAYANI SHINYANGA WAADHIMIA KUTOHUDUMIWA MAJI NA SHUWASA


Baraza la madiwani wa Halmshauri ya wilaya Shinyanga limeadhimia kwa kauli moja ya kutohudumiwa na Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) na badala yake kuhudumiwa na Wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijiji (RUWASA) kutokana na kuuziwa bei kubwa kwa Unit moja ya maji.

Wameazimia hayo leo Mei 10, 2024, wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kujadili ajenda mbalimbali amoja nakupokea taarifa kutoka taasisi mbalimbali.

Wametoa kauli hiyo kutokana na kero ya muda mrefu hiyo kuwa ya muda mrefu hasa kwa kata Didia tangu mwaka 2022 ankara za maji kuwa na bei kubwa ukilinganisha na maeneo mengine ya halmshauri hivyo kutoa kauli ya pamoja ya kutokudumiwa na Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).
Akiwasilisha kero wakati wa kikao hicho Diwani wa kata ya Didia Richard Masele amesmea amelalamikia bei kubwa ya maji wanayotozwa wananchi wa kata ya Didia licha ya suala hilo kupatiwa ufumbuzi na mkuu wa wilaya lakini bado haijabadilishwa.
“Wakati tunahamishwa kutoka RUWASA kwenda SHUWASA binafsi sikukubaliana na suala lile kwasababu sikuwa na uhakika kuwa tutakwenda kunufaika na ndio yanayojitokeza sasa kijiji cha Mwanono na Mwamalulu kwenye kata ya Didia havina maji, mimi maendekezo yangu nani maombi ya wananchi kwa niaba ya wananchi kama wameshindwa kutuhudumia waturudishe kule tuliokuwa tuliokuwa RUWASA hatukuwa na malalamiko haya”, amesema Diwani Masele.
“Mheshimiwa mkuu wa wilaya alizungumza na mkurugenzi wa EWURA na kukubaliana kuwa bei hiyo ibadilishwe lakini mpaka leo hakuna mabadiliko yeyote juu ya bei hizo nikuombe mheshimiwa mwenyekiti kupitia baraza hili tupate azimio la pamoja juu ya suala hili”, ameongeza Diwani Masele.

Diwani wa Kata ya Iselamagazi Isack Sengerema amekiri kupokea taarifa kutoka Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) juu ya kupanda kwa bei ya maji kwenye kata yake kutoka Sh. 1,000/= hadi Sh. 2,550/=.

“Jambo hili ni gumu sana kwa sababu maji ni huduma lakini SHUWASA wamefanya kuwa biashara haiwezekani bei ya maji ilingane sawa na bei ya Petrol ambayo yanasafirishwa kutoka nje ya nchi, hata mimi nimepokea taarifa ya kupanda kwa maji kutoka Sh. 1,000/= hadi Sh. 2,550/=.yani sis indo tunakwenda kulipa bei kubwa kuliko sehemu zote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboji amesema kutokana na malalamiko yaliyotolewa na madiwani juu ya bei kubwa ya maji kwenye baadhi ya maeneo ndani ya halmashauri hiyo ameiomba ofisi ya mkuu wa wilaya Shinyanga Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) isitishe kutoa huduma kwa wananchi waishio vijijini amoja na kutoa kauli ya baraza juu ya suala hilo.
“Nikuombe ofisi ya mkuu wa Wilaya pamoja na mazungumzo yako mazuri na wizara Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) hawatakiwi kuhudumia maeneo ya vijijini kwasababu ya kero inayoonekana, Sh 2,550/= kwa maisha ya mwananchi wa kawaida anaeishi kwenye nyumba ya nyasi hawezi kumudu gharama hizi, sisi kama baraza tunaiomba ofisi ya mkuu wa wilaya iwaondoshe Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) wabaki maeneo ya mjini sehemu zilizo na mzunguko wa fedha lakini kwetu sisi kama baraza la madiwani hili ni azimio kuwa hatuwahitaji” , amesema Ngasa Mboji.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ambaye ni kaimu meneja kanda ya Iselamagazi Martini Shemgaa amesema zipo taratibu za upangaji wa bei kulingana na maeneo husika na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo ili kuendeea kutoa huduma kwa wateja wao.

Awali akisoma taarifa ya robo tatu ya mwaka 2023/2024 kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Sitewart Makali mbali na masuala mbalimbali yakimaendeleo ia amebainisha uwepo wa mliuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
"Halmashauri yetu imeokea taarifa ya uweo wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo tarehe 30/04/2024 jumla ya watu 11 waligundulika kuambukizwa ugojwa huo katika kata ya Mwakitolyo, ambapo watu wawili walifariki wengine 9 walipatiwa matibabu na kuruhusiwa", amesema Sitewart Makali.

‘Kufuatia mlipuko huo halmashauri imechukuwa hatua za kukabiliana na ugonjwa huo kwa kugawa dawa za kutibu maji kwa kaya 462, kutibu visima vya maji 16 na kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu’, ameongeza Sitewart Makali.

Baadhi ya madiwani wakati wa kikao hicho
Mwakilishi wa mkuu wa wilaya Aaron Laizer akizungumza wakati wa kikao hicho.
Naibu Afisa msaidizi uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Lidya Mwamsiku akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani.
Kaimu meneja wa Wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijiji (RUWASA) wilaya ya Shinyanga Nkinda Senni akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboji akizungumza wakati wa kikao hicho.
Diwani wa kata ya Itwangi Sonya Jilala akizungumza wakati wa kikao hicho.


Diwani wa kata ya Ilola Amos Mshandete akizungumza wakati wa kikao hicho.
Diwani wa kata ya Imesela Seth Msangwa akizungumza wakati wa kikao hicho.
Diwani kata ya Solwa Hawadh Hafiz akizungumza wakati wa kikao hicho.

Post a Comment

0 Comments