Header Ads Widget

SHY WOMENS JOURNALIST WAZINDUA RASMI UMOJA WAO,WAAHIDI KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUKUZA UCHUMI

baadhi ya waandishi wa habari wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja

Na Suzy Luhende,Shinyanga Press Club Blog

Waandishi wa habari wanawake Mkoani Shinyanga (Shy Women's Journalist) wamezindua rasmi Umoja wao kwa ajili ya kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kusaidiana katika shida na raha, ikiwa ni pamoja na kutembelea watu wenye mahitaji maalumu,yatima na wajane.

Uzinduzi huo umefanyika Mjini Shinyanga kwa lengo la kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia taaluma yao kwa kuibuwa na kuanzisha miradi itakayowawezesha kujikwamuwa kiuchumi na kusaidiana katika shida na raha na kutumia fursa mbalimbali zilizopo.

Mwenyekiti wa Waandishi wa habari wanawake Moshi Ndugulile, amesema umoja huo utasaidia kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo, kutembelea watoto yatima, wazee na makundi yenye mahitaji maalumu pamoja na kupata uzoefu kutoka kwa wanawake ambao wamefanikiwa zaidi.

"Sisi waandishi wa habari wanawake Mkoa wa Shinyanga tumeamua kuanzisha umoja wetu kwa ajili ya kushirikiana masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kutembea watu wenye mahitaji maalumu, kwani sisi wanawake ni jeshi kubwa tunaweza kufanya mambo makubwa katika jamii yetu " amesema Ndugulile.

Katibu wa waandishi wa habari wanawake Stella Ibengwe,amewaomba waandishi wa habari wanawake kuimarisha umoja wao hatua ambayo itawawezesha kupiga hatua zaidi na kuwa na mafanikio makubwa,huku akiwapongeza kwa hatua hiyo ya uzinduzi kwani ni njia ya mafanikio.

Baadhi ya wajumbe wa Umoja huo akiwemo Elizabeth Charles na Suzy Butondo wamewaomba waandishi wanawake wadumishe upendo katika umoja wao, huku wakimtegemea Mungu aweze kuwasimamia kwa kila jambo wanalotaka kulifanya ili liweze kufanikiwa.

"Leo tumezindua Umoja wetu kwa pamoja, tunafuraha sana hivyo niwaombe tushirikiane kwa pamoja na tumshirikishe Mungu aweze kutusimamia kwa kila jambo tunalotaka kulifanya na tuhakikishe kila tunalolipanga linafanikiwa,"amesema Butondo

Keki iliyotengenezwa kwa umakini zaidi  na mwandishi wa Star Tv Elizabeth Nyanda kwa ajili ya Shy Womens Journalist 
Mwenyekiti wa Shy Womens Journalist akikata keki 
Katibu wa Waandishi wanawake Stella Ibengwe akimlisha keki Airine Kishiwa mwandishi wa Jambo Fm 

Katibu wa Waandishi wanawake Stella Ibengwe akimlisha keki Kareny Masasy 
Katibu wa Waandishi wanawake Stella Ibengwe akimlisha keki Mwenyekiti wa Umoja wa waandishi wa habari wanawake
Katibu wa Waandishi wanawake Stella Ibengwe akimlisha keki Mwandishi wa habari Suzy Butondo
Waandishi wanawake wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali
Waandishi wanawake wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali
Waandishi wanawake wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali
Waandishi wanawake wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali

Waandishi wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja 
Waandishi wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja 


Waandishi wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja 
Waandishi wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja 
Waandishi wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja 
Waandishi wanawake wakiwa kwenye picha ya pamoja 


























Post a Comment

0 Comments