Header Ads Widget

SHIRIKA LA COMPASSION INTERNATIONAL KLASTA YA IGUNGA LAGAWA VITABU MASHULENI KUADHIMISHA MIAKA 25


Mkurugenzi wa Vituo vya huduma ya mtoto Klasta ya Igunga Manase Silasi akizungumza na wanafunzi

        Na stella Homolwa,Shinyanga Press Club Blog

 Shirika la Compassion International Tanzania Klasta ya Igunga limeadhimisha miaka 25 ya Shirika hilo,kwa kutoa msaada kwa makundi mbalimbali,vikiwemo vitabu na vifaa vya michezo kwa shule za Msingi.

  Mkurugenzi wa Vituo vya huduma ya mtoto Klasta ya Igunga Manase Silasi  amesema katika maadhimisho hayo pia wameshiriki katika usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema Shirika la Compassion International kwa Wilaya ya Igunga linahudumia watoto zaidi ya 800 kupitia kwenye Vituo vyake ambapo wanawawezesha kuwajenga kiimani na kuwapatia huduma zote muhimu ikiwemo elimu,matibabu na kuhakikisha wanakaa kwenye mazingira mazuri.

 Amesema wamegawa Vitabu na vifaa vya michezo katika shule mbalimbali za Wilaya ya Igunga ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 25 ya Compasion katika   vituo vya huduma na  maendeleo ya mtoto na kijana Klasta ya Igunga Mkoani Tabora.

Mkurugenzi wa vituo vya huduma ya mtoto klasta ya Igunga Manase Silasi amesema wameamuwa kuadhimisha miaka 25 ya shirika la Compassion kwa kuwafikia wanafunzi pamoja na kusisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu katika jamii.

Wakizungumza baada ya kukabidhi vitabu na vifaa vya michezo baadhi ya viongozi wa dini na walimu wamesema kuna  umuhimu wa kuwekeza katika elimu na kusisitiza suala la maadili kwa vijana kutokana na kuwa na utandawazi na watu kufanya vitendo vya ukatili.


 



                        Zoezi la kugawa vitabu likiendelea


          








Post a Comment

0 Comments