Header Ads Widget

WASICHANA 198,865 KUCHANJWA CHANJO SARATANI YA MLANGO WA SHINGO YA KIZAZI SHINYANGA HPV

Wasichana 198,865 kuchanjwa Chanjo Saratani Mlango Shingo ya kizazi Shinyanga

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKOA wa Shinyanga katika kampeni ya utoaji wa Chanjo ya HPV dhidi ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi, unatarajia kuwachanja Wasichana 198,865 wenye umri kuanzia miaka 9 hadi 14.
Kampeni hiyo ya Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi mkoani Shinyanga, inatarajia kuanzia Aprili 22 hadi 28, na pia utoaji huo wa Chanjo utakuwa endelevu hadi Decemba mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,akizungumza leo April 19,2024 kwenye kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,amesema utoaji wa Chanjo hiyo kwa wiki moja utawafikia Wasichana 198,865 wenye umri kuanzia miaka 9 hadi 14.

"Utoaji wa Chanjo hii ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi, ni kuongeza kinga kwa Wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 dhidi ya ugonjwa huo, natoa wito kwa wazazi waruhusu Mabinti zao wapate Chanjo hii, ili kulinda Afya za watoto wao,"amesema Mkude.
Aidha,ametoa Maagizo pia kwa viongozi wa Serikali wakiwamo Watendaji wa Kata,na Vijiji kuwabaini pia wasichana ambao hawapo mashuleni ili waweze kupata Chanjo hiyo.

Amewaagiza pia Wataalamu wa Afya watakatoe Elimu ya Chanjo hiyo ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi kwenye nyumba za Ibada.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Yudas Ndungile, amesema utoaji wa Chanjo hiyo ya HPV dhidi ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi, ilianza kutolewa Mwaka 2014 kwa kutolewa kwa dozi mbili, lakini sasa hivi kutokana na Mabadiliko itatolewa kwa dozi Moja.

"Tafiti za Kisayansi zimethibitisha kuwa dozi Moja ya Chanjo ya HPV inatosha kutoa kinga kamili dhidi ya Maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya Kizazi,"amesema Ndungile.
Naye Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Shinyanga Timothy Sosoma, amesema Chanjo hiyo ya Saratani ya Mlango ya Shingo ya Kizazi, itatolewa Shuleni kwa shule zote za Msingi na Sekondari 887pamoja na kwenye Vituo vya Afya 241.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Paul Julius, ameupongeza Mkoa wa Shinyanga, kutokana na Maandalizi Mazuri ya Utoaji Chanjo hiyo ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi,kwamba ametembelea baadhi ya maeneo ambapo vitendea kazi vya utoaji Chanjo hiyo vimeshafika maeneo husika.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Post a Comment

0 Comments