Header Ads Widget

KATAMBI,SANTIEL WATOA NG’OMBE WA CHRISTIMAS MAGEREZA WILAYA YA SHINYANGA

KATAMBI,SANTIEL WATOA NG’OMBE WA CHRISTIMAS MAGEREZA WILAYA YA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, pamoja na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba, wametoa Ng’ombe wa Christimas Magereza ya wilaya ya Shinyanga.

Ng’ombe huyo amekabidhiwa leo Decemba 24, 2023 na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson kwa niaba ya Wabunge hao, kwa Mkuu wa Magereza ya wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi, pamoja na Sh.Laki 2 iliyotolewa na Mbunge Katambi kwa ajili ya kununua Sabuni za kufulia.
Samweli akizungumza wakati wa kukabidhi Ng’ombe na fedha Sh.Laki 2, amesema Mbunge Katambi na Santiel, waliahidi kutoa Ng’ombe kwenye Magereza hiyo ya wilaya ya Shinyanga, na leo wametekeleza ahadi yao ili Askari Magereza pamoja na wafungwa washerehekee Siku Kuu ya Christimas kwa furaha na upendo.

“Mbunge Katambi pamoja na Santiel waliahidi kutoa Ng’ombe wa Christimas katika Magereza hii ya wilaya ya Shinyanga, na wametekeleza ahadi yao na thamani ya Ng’ombe huyu ni Sh, Laki 7, nimekabdhi pia na Sh.Laki 2 ambazo zimetolewa na Mheshimiwa Katambi kwa ajili ya kununua sabuni za kufulia ni moja pia ya ahadi yake kwa wafungwa,”amesema Samweli.
“Mheshimiwa Katambi na Santiel wanawatakia Askari Magereza na wafungwa wote, heli ya Siku Kuu ya Christimas na Mwaka Mpya 2024,”ameongeza Samweli.

Naye Mkuu wa Magereza ya wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi, amewashukuru Wabunge hao kwa zawadi hiyo waliowapatia ya Ng’ombe kwa ajili ya Siku Kuu ya Christimas na kutekeleza ahadi yao, pamoja na fedha Sh.Laki 2 ya kununua Sabuni za kufulia nguo za wafungwa, na kutoa wito pia kwa viongozi wengine wawe wanawakumbuka na wafungwa katika Sherehe mbalimbali.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson (kushoto) akikabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga aliyetolewa na Wabunge Katambi na Santiel Kirumba, (kulia)ni Mkuu wa Magereza hiyo Theophil Mulokozi.
Zoezi la kukabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwil Jacskon (kushoto)akibidhi Sh. Laki 2 kwa Mkuu wa Magereza wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi pesa iliyotolewa na Mbunge Katambi kwa ajili ya kununua Sabuni za kufulia.
Picha ya pamoja ikipigwa.


Post a Comment

0 Comments