Header Ads Widget

WAWEKEZAJI KWENYE VYUO VYA AFYA WAMESHAURIWA KUWEKA KOZI ZOTE ILI KUENDANA NA SOKO LA AJIRA





Wahitimu  wa chuo cha sayansi ya afya Kahama wakijiandaa kuingia ukumbini.

 Na Kareny  Masasy,

Kahama

TAASISI binafsi zinazowekeza kwenye vyuo vinavyotoa  taaluma mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya afya kwa binadamu zimeshauri  kuweka na kozi  ambazo wataalamu wake wachache ili kuendana na  soko la ajira.

Hayo yamesemwa leo tarehe 10/08/2023 na mgeni rasmi Mdoe Ibrahimu ambaye  ni kaimu mkurugenzi wa mafunzo kutoka wizara ya afya  akimwakilisha  naibu waziri wa Afya  Godwin Mollel kwenye mahafali ya saba katika chuo cha  sayansi  za afya  Kahama (KACHS).

Ibrahimu amesema kuna vyuo 219 vinavyotoa taaluma ya masuala ya afya ambapo vyuo vya serikali ni 43 tu hivyo serikali imejitahidi kutoa ajira kwa waliohitimu ufamasia na utabibu lakini kuna changamoto za kozi zingine  kama uungaji wa viungo vya mwili kama umepata ajali na afya ya akili  wanahitajika wataalamu.

Ibrahimu amesema wahitimu wanaomaliza wakiwa wanasubiri ajira wajikite kwenye masuala mengine wakipata fursa wasikae tu mitaani na waendelee kuielimisha jamii  na wakipata ajira waitumie vizuri wasiwe chanzo cha kukosa maadili.

“Wakufunzi  nanyinyi  muwafundishe namna ya uvaaji  na kujiweka utakuta mtumishi wa afya kucha ndefu kapaka rangi, koti na suruali vimebana nywele mitindo ya siku hizi kama mwanamziki taaluma haitaki mambo hayo”amesema Ibrahimu.

Ibrahimu amesema suala la vyuo vya kati wanafunzi kupata mkopo kama vyuo vingine hilo lilijadiliwa bungeni na baadhi ya wabunge walitoa mapendekezo  na serikali ililichukua hivyo utaratibu ukiwepo umma utajulishwa.

Mkurugenzi wa chuo hicho Yona Bakungile amewapongeza walimu kutoa mafunzo kwa wahitimu kwani mafunzo haya ya afya ni magumu  na ukiona kijana kamaliza  ni jambo la kumshukuru mungu kwani wapo walirudia mwaka jana walifeli,wapo waliougua na wapo waliokatiza masomo sababu ya ada.

“Ninyi wahitimu  mkipata ajira muende mkawatumikie wananchi kwa kuisadia serikali  na shule za sekondari zimejengwa kila kona zikimaanisha vyuo kupata wanafunzi hivyo aliomba serikali kuwapatia mkopo wanafunzi kwani wao hawapati ruzuku ikitokea  mwanafunzi ameshindwa kulipa ada basi chuo hakina namna”amesema Bakungile.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu Aloyce Mzaga amesema  wameweza kumudu masomo  hivyo wanaahidi kwa serikali  pindi wakipata ajira kuitumia vyema taaluma hiyo  ambapo wahitimu wa ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii,tabibu na ufamasia ni 162.

“Chuo hicho kilianza mwaka 2016 kinajikita katika  mafunzo yenye ubora na changamoto inayotukumba  ni baadhi ya wanafunzi kukatiza masomo sababu ya ada hivyo tunaiomba serikali kutupatia mkopo sisi wanafunzi tuliopo  kwenye vyuo vya kati”amesema Mgaza.

Mkurugenzi wa chuo cha Sayansi  na Afya Kahama  Yona Bakungile akiongea siku ya Mahafali ya saba ya chuo hicho.

Mkuu wa chuo cha sayansi ya Afya Kahama Vivian  Mpangalala akitambulisha  wageni waalikwa siku ya mahafali chuo hicho.

Mgeni rasmi  Mdoe Ibrahimu ambaye ni kaimu mkurugenzi wa mafunzo kutoka wizara ya afya akimwakilisha naibu waziri wa Afya.  siku ya Mahafali ya saba katika chuo cha sayansi na Afya  Kahama  akitoa neno kwa wahitimu na kukishauri chuo hicho.



Mwanafunzi Aloyce Mgaza akiwa maabara ya kujifunzia kwa vitendo ambaye anahitimu.

Wanafunzi wa chuo wakiwa katika maabara ya kujifunza kwa vitendo.





Wanafunzi wa chuo cha  sayansi na Afya  Kahama wakimpima mmoja wa wateja aliyejitokeza kupimwa.

Wanafunzi wakisubiri kutoa maelezo kwa mgeni rasmi

Wanafunzi wakiwa maabara ya kujifunzia

Walimu  wa chuo cha sayansi na Afya Kahama .

Wageni waalikwa katika mahafali ya chuo.






Post a Comment

0 Comments