Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA WAPEWA ELIMU JUU YA UTAMBUZI WA SHERIA YA USIMAMIZI WA KODI 2015 KWA KUTAFSRIWA.





 Mwenyekiti wa TCCIA wilayani Kahama akitoa neno mbele ya wafanyabiashara  baada ya  mafunzo ya  usimamizi wa sheria ya kodi  ya mwaka 2015.

Na Kareny  Masasy, Kahama

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)  Mkoa wa kikodi Kahama  imetoa Elimu juu ya tafsiri  ya Sheria  ya Usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 kwa lugha  ya Kiswashili   ili kuwa na urahisi wa wafanyabiashara kuzielewa na kulipa kodi kwa wakati.

Kaimu meneja   kutoka mamlaka hiyo   Honest  Mush ambaye  ni meneja msaidizi   anayeshughulikia  kaguzi za kodi  amesema  hayo jana wakati wa  utoaji elimu kwa wafanyabiashara juu ya  sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015.

Mushi amesema Tafsiri ya Sheria hizi Wafanyabiashara zinawahusu  ambapo ameelezea  kifungu 37 cha Sheria ya Usimamizi wa kodi kinachohusu  uwasilishaji wa ritani ya kodi ambapo mlipaji binafsi au kampuni kukiri kuwa mwaminifu na ulipaji usio danganya au uliosahihi.

Mushi amesema kifungu cha Sheria namba 75  kinachoeleza Riba na  Adhabu  mbalimbali  za makosa ya kikodi   yatatokana na kukokotolewa  kwa kosa la kufanya makadirio ya chini ya kodi halisi inayohitajika.

Mushi amesema  kifungu namba 77 cha Sheria  kinaeleza atakaye shindwa kutunza kumbukumbu za biashara Adhabu kwa kampuni   na adhabu ya kushindwa kuwasilisha  Ritani ya kodi  kwa wakati ikiwa  itakatwa asilimia 2.5 ya kodi iliyokadiriwa kwenye ritani.

 “Nimetafsiri Sheria hizi kwa lugha ya Kiswahili ambayo itaeleweka kwa wote  lengo ninataka na ninyi mzielewe kama ninavyoelewa mimi nakusiwepo ukwepaji wa kodi usio na sababu za msingi.”amesema Mushi.

Mushi amesema Malengo  wamepagiwa  ulipaji kodi mwaka wa fedha 2022/2023 sh Billioni 18  na tangu walivyapangiwa wamekusanya sh Billioni 10 mpaka kufikia mwezi Julai watafikisha malengo hayo.

Ofisa wa kodi kutoka TRA Godfrey Chama amesema  kodi hutozwa kwa wafanyabiashara wakubwa kwa kuangalia faida ila wafanyabiashara  wadogo huangalia mauzo kipindi cha  Januari hadi March    kila  mfanyabiashara  anapaswa awe amekadiriwa kodi yake.

Ofisa Elimu kwa Mlipakodi Anceth  Ndailagije  amesema  ulipaji kodi unafuata Miongozo na  Sheria ambapo kuna kukadiriwa, kukusanya,kusimamia na kuinua kiwango cha mlipakodi na kuboresha hali ya walipa kodi na kuzuia ukwepaji kodi.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara,viwandani  na Wakulima (TCCIA)  Wilayani Kahama Charles Machali alisema    sheria hizo wametafsiriwa na kugawiwa na matumaini watakwenda kufanyia kazi nakulipa kodi kikamilifu.



Wafanyabiashara  wilayani Kahama wakiwa kwenye mafunzo ya elimu ya mlipakodi

Wafanyabiashara wakiwa katika mafunzo juu ya elimu ya mlipa kodi

Kaimu meneja mkoa  kutoka  TRA mkoa wa kikodi Kahama  Honest  Mush ambaye  ni meneja msaidizi   anayeshughulikia  kaguzi za kodi akitoa elimu.

Kaimu meneja mkoa  kutoka TRA mkoa wa kikodi Kahama  Honest  Mush ambaye  ni meneja msaidizi   anayeshughulikia  kaguzi za kodi 

Mwenyekiti wa TCCIA wilaya ya Kahama Charles Machali na kaimu meneja wa TRA  mkoa wa kikodi Kahama Honest Mushi wakiwa meza kuu

Afisa mlipa kodi kutoka Malmlaka ya Mapto TRA mkoa wa kikodi Kahama  Godfrey Chama akitoa elimu


Wafanyakazi wa mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa kikodi Kahama wakifanya maadalizi ya utoaji elimu

Post a Comment

0 Comments