Header Ads Widget

MTANDAO WA POLISI WANAWAKE WATOA MSAADA KWENYE KITUO CHA KULELEA WAZEE KOLANDOTO

 Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiongea kwenye kambi ya wazee wa Kolandoto baada ya kupeleka msaada,

Na  Marco Abel, Shinyanga

MTANDAO  wa polisi wanawake mkoa Shinyanga wamefanya matembezi na kutoa msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwenye kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza kilichopo kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga.

 Mtandao huo umetoa msaada  tarehe 07/03/2023 katika maadhimisho kuelekea siku ya wanawake duniani ifikapo March 8 mwaka huu kwenye kituo cha malezi ya wazee wasiojiweza, Kolandoto  mkoani Shinyanga.

 Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake mkoa wa shinyanga ambaye pia ni kamanda wa polisi mkoani humo ACP. Janeth Magomi amesema wameamua kutoa msaada huo ili kuonyesha upendo na kuwathamini wazee hao kwani kwa kufanya hivyo inawatia moyo na kuona namna serikali na watu wengine wanavyothamini uwepo wao.

 “Kulelekea siku ya mwanamke duniani sisi kama mtandao wa polisi wanawake mkoa wa Shinyanga tumeona tufike kwenye kituo cha malezi ya wazee wasiojiweza ili kuonyesha thamani yao kwetu na kutambua uwepo wao, tumefurahi kujumuika nanyi siku ya leo”, ameseam Magomi. 

 mratibu wa kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza kolandoto  Sophia Kang’ombe amesema wameendelea kutoa huduma za malazi, chakula na matibabu kwa wazee hao licha ya idadi yao kupungua, “Kipindi cha nyuma tulikuwa na idadi kubwa ya wazee lakini kutokana na jitihada za serikali kuwaunganisha wazee hawa pamoja na ndugu zao hadi sasa wameweza kupungua na kufikia wanaume 11 na wanawake 5”, amesema Sophia Kang’ombe.

 

Naye mwenyekiti wa makazi ya wazee kituo cha kolandoto Kija Nipuge akawashukuru Mtandao wa polisi wanawake mkoa Shinyanga  kwa kuwatembelea na kutoa msaada kituoni hapo na kuomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono kitu hicho. 

Post a Comment

0 Comments