Header Ads Widget

SHINYANGA WAJIVUNIA MAFANIKIO MIAKA MIWILI YA UTAWALA WA RAIS SAMIA,MIRADI KIBAO YA MAENDELEO YATEKELEZWA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia mkoani Shinyanga ikiwamo utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKOA wa Shinyanga wamefanya Kongamano la miaka miwili ya mafanikio ya Utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kongamano hilo limefanyika leo Machi 25, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiwamo na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, akielezea mafanikio ya Mkoa huo wa Shinyanga ndani ya miaka miwili ya Rais Samia, amesema zimeletwa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Akielezea mafanikio katika Sekta ya Afya, amesema Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 32.6 na kujengwa vituo mbalimbali vya Afya na Zahanati, pamoja na Sh.bilioni 7.8 kujengwa Hospitali ya Rufaa mkoani humo, na kuondoa adha ya wananchi kufuata huduma za matibabu Bugando Jijini Mwanza na Mhimbili.

Amesema pia Rais Samia katika Mkoa huo ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 14.9 na kununua Vifaa Tiba pamoja na Madawa na katika Mkoa huo kuna upatikanaji wa Madawa asilimia 89.

Akizungumzia Sekta ya Elimu amesema Rais Samia ametoa fedha Sh.bilioni 37.6 na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwamo ujenzi wa matundu ya vyoo, madawati, vyumba vya Madarasa, huku akitoa fedha zingine na kujengwa Chuo cha VETA wilayani Kishapu, pamoja na Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana iliyopo Butengwa Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumzia mafaniko katika Sekta ya Maji, amesema Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 52.2 na kutekelezwa Miradi ya Maji 45, na katika mwaka wa fedha (2021/2022) RUWASA ilipokea Bilioni 29.5 na kutekelezwa miradi ya maji 29, pia kuna ujenzi wa miradi mipya ya maji 15 yenye thamani ya Sh.bilioni 24.3.

Amesema pia katika mwaka wa fedha (2022/2023) RUWASA Mkoa walipokea fedha Sh.bilioni 22.7 na kutekelezwa miradi ya maji 15 na kuondoa adha ya wananchi kutumia maji yasiyofaa.

Ameelezea mafaniko ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara, amesema katika utawala wake Rais Samia ndani ya miaka miwili, zimejengwa barabara nyingi ikiwamo ujenzi wa Makaravati, Madaraja pamoja na uwekaji wa Taa za Barabarani.

“Mkoa wa Shinyanga ndani ya miaka miwili ya utawala wa Rais Samia tunajivunia mafaniko makubwa ya kimaendeleo pamoja na mapinduzi ya kiuchumi, ikiwamo na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),”amesema Mndeme.

“Rais Samia ametoa tena fedha Sh.bilioni 21 kwa ajili walengwa wa mpango wa kunusuru Kaya maskini TASAF, huku zikitolewa Lesseni za uchimbaji madini 827 na Lesseni za wachimbaji wadogo 267,”ameongeza Mndeme.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amempongeza Rais Samia kwa kutekeleza ilani ya Chama hicho kwa vitendo, na wameona mvua kubwa ya maendeleo na wataendelea kumuombea afya njema ili aendelee kuwatumikia vyema watanzania.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pi ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwa niaba ya Wabunge wote wa Mkoa huo, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi katika Mkoa huo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia mkoani Shinyanga ikiwamo utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia wilayani Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia wilayani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia wilayani Kahama.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga Mabala Mlolwa akielezea namna Rais Samia alivyotekeleza ilani ya CCM kwa vitendo mkoani Shinyanga na kutekelezwa miradi mingi ya maendeleo.
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava akielezea mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye ulemavu akielezea mafaniko ya miaka miwili ya Rais Samia katika utawala wake.
Viongozi wakiwa kwenye kongamano la mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye ulemavu (kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo kwenye Kongamano la miaka miwili ya mafanikio ya Rais Samia mkoani Shinyanga.
Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa wakiwa kwenye Kongamano la miaka miwili ya mafanikio ya Rais Samia Mkoani Shinhyanga.
Kongamano la miaka miwili ya mafanikio ya Rais Samia mkoani Shinyanga likiendelea.

Burudani ikitolewa kwenye Kongamano hilo la miaka miwili ya Rais Samia mkoani Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments