Header Ads Widget

HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA IMEFANYA KIKAO CHA ROBO MWAKA CHA UTEKELEZAJI SHUGHULI ZA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Kikao cha Robo mwaka cha utekelezaji wa shughuli za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

HALMASHAURI ya wilaya ya Shinyanga, imefanya kikao cha Robo mwaka cha utekelezaji wa shughuli za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kikao hicho kimefanyika leo Machi 20, 2023 katika Makao Makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga yaliyopo Kata ya Iselamagazi, na kuwasilishwa taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga matukio ya ukatili kutoka mashirika mbalimbali, ambayo yalikuwa yakitekeleza mradi huo wilayani Shinyanga kwa kipindi cha miezi mitatu, kwa ufadhili wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust).

Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani Shinyanga Joram Magana, akizungumza kwenye kikao hicho amesema Mashirika yasiyo kuwa ya Kiserikali yamekuwa na mchango mkubwa kupunguza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga.

Amesema Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa sasa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yamepungua kwa kiasi kikubwa, ambapo jamii imekuwa na uelewa mkubwa wa madhara ya kufanya ukatili, kutokana na elimu kutolewa ipasavyo kwa wananchi.

Naye Katibu wa Mpango Mkakati wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga Aisha Omary, amesema mradi huo umekuwa na mafaniko makubwa, ambapo jamii wamekuwa wakichukuliana hatua wao wenyewe kwa wale ambao wanafanya ukatili.

“Tuna ushukuru Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) kwa kufadhili na kutekelezwa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa wilayani Shinyanga ambao umesaidia kupunguza ukatili wa wanawake na watoto,”amesema Aisha.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Ofisa Oparation kutoka Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Emmanuel Galiyamoshi akimwakilisha Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Janeth Magomi, amewapongeza wadau wa maendeleo kwa kufanya kazi kubwa ya kupinga matukio ya ukatili, na kuahidi Jeshi litaendelea kushirikiana nao ili kukomesha matukio hayo.

Aidha, ametaja baadhi ya Changamoto ambazo wanakabiliana nazo ikiwamo ufinyu wa chumba katika vituo vya Polisi, kwa ajili ya kuhifadhi Madhura ambao wanafanyiwa vitendo vya ukatili na kusababisha kuharibika kwa Ushahidi, sababu binti akirudi kwao anarubuniwa na wazazi na kumkana mtuhumiwa ambaye alimtaja awali kuwa kampatia ujauzito.

Nayo Mashirika ambayo yaliwasilisha taarifa zao za utekelezaji wa Mradi wa kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani Shinyanga kwenye kikao hicho cha Robo mwaka, wametaja mafanikio kwamba jamii imekuwa na uwelewa mkubwa wa kupinga ukatili, na wamekuwa wakitoa taarifa za viashiria vya ukatili pamoja na watu ambao wameshafanyiwa ukatili na kuzifanyia kazi.

Mashirika ambayo yalipata ufadhili wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) ambayo yamewasilisha taarifa zao za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga kwenye kikao hicho cha Robo mwaka, kuwa ni Thubutu Africa Intiatives, Young Women Leadership (YWL) WEADO, Rafiki SDO, GCI, YAWE, pamoja na Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi, Shinyanga Press Club, na Radio Faraja.
Ofisa Oparationi kutoka Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Emmanuel Galiyamoshi akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani Shinyanga Joram Magana, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mganga wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa MTAKUWWA wilayani Shinyanga Aisha Omary akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga Estormine Henry akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Msimamizi wa vipindi Radio Faraja Simeo Makoba akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Afisa Miradi kutoka Shirika la GCI Ngolelwa Masanja akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa Mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Paschalia Mbungani kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiatives akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Paul Julius kutoka Shirika la Rafiki SDO akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Afisa Miradi kutoka Shirika la YAWE Moshi Jilalage akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Monica Shehere akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
John Eddy kutoka Shirika la WEADO akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Veronica Masawe kutoka Shirika la YWL akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza la watoto Kata ya Iselamagazi Elias Yohana akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza la watoto Kata ya Puni Amina Hamisi akizungumza kwenye kikao hicho.
Meza kuu wakiwa kwenye kikao cha Robo mwaka cha usikilizaji wa taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Meza kuu wakiwa kwenye kikao cha Robo mwaka cha usikilizaji wa taarifa za utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye kikao hicho.

Post a Comment

0 Comments