Header Ads Widget

WANAWAKE WACHIMBAJI WA MADINI WAJENGA ZAHANATI KUSAIDIA WAKINAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO.


Jengo la zahanati ambalo limejengwa na wanawake wachimbaji wa madini katika mgodi wa Nyamishiga Kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga kupitia kikundi cha Mshikamano Tawoma.
Na Shinyanga press club blog 

Wanawake wachimbaji wadogo wa madini kikundi cha Mshikamano (Tawoma) katika mgodi wa Nyamishiga Kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama,wamejenga jengo la zahanati kijiji cha Nyamishiga hatua itakayosaidia kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu Lunguya.

Mwenyekiti wa wachimba wa madini wanawake Tanzania,ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano Tawoma mgodi mdogo wa Nyamishiga Semeni John,amesema ujenzi wa zahanati hiyo pamoja na nyumba ya Daktari fedha zake zinatokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini wanawake ambazo zinakwenda kusaidia huduma za jamii.

Amesema tayari Sh Milioni 203 zimetolewa na wanawake wachimbaji wa madini ambazo zinatumika kwenye ujenzi wa zahanati,vyoo,na nyumba ya Daktari hatua ambayo itasaidia kupunguza changamoto zilizopo kutokana na Kijiji hicho kutokuwa na huduma za afya ambapo wananchi wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda kituo cha afya Lunguya.

“Tangu tumeanza usimamizi wa mgodi huu sisi wanawake tumeiingizia mapato serikali zaidi ya Sh Bilion mbili ambapo pia tumejenga zahanati itakayosaidia kutoa huduma kwa wananchi,na wachimbaji wadogo wa madini ambao wengi wako katika eneo hilo wakiendelea na shughuli zao za kila siku”alisema Semeni John Mwenyekiti wa Tawoma.

Katibu wa Kikundi cha Tawoma Hilda Busomelo amesema zahanati hiyo atasaidia wakina mama wajawazito na watoto kupata huduma karibu badala ya kutembea umbali mrefu kupeleka watoto kliniki na kwenda kwenye matibabu.

Amesema mbali na kusaidia huduma za jamii lakini pia wamekuwa wakitoa msaada kwa wazee wasiojiweza ili kuwawezesha kujikimu kimaisha pamoja kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo.

Wanawake hao wachimbaji wadogo wa madini pia wameiomba serikali kupitia wizara ya madini kuwarasimisha na kuwapatia leseni za uchimbaji mdogo kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi na kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali.


Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji wadogo wa madini Tanzania ambape pia ni Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wachimbaji wa madini Mshikamano mgodi wa Nyamishiga Semeni John


Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Mkoa wa Shinyanga Hamza Tandiko akizungumza baada ya kutembelea mgodi wa Nyamishiga


 
Afisa madini Mkoa wa kimadini Kahama Jeremia Hango akizungumza katika mgodi mdogo wa Nyamishiga


  Wakinamama wakiendelea na shughuli zao mgodini


       Wachimbaji wakiendelea na shughuli zao
Katibu wa kikundi cha Mshikamano cha wanawake wachimbaji wa madini Hilda Busomelo akiendelea na shughuli mgodini
                      shughuli zikiendelea
                             

            Mifuko ya mawe ya madini ya Dhahabu imeandaliwa kwa ajili ya kuchukuliwa na wachimbaji

     
                        Zoezi likiendelea
 
          Baadhi ya viongozi wa wachimbaji  wa madini wanawake


            

Baadhi ya viongozi wakikagua ujenzi wa vyoo katika zahanati mpya inayojengwa Kijiji cha Nyamishiga


       Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji wadogo wa madini Tanzania




Post a Comment

0 Comments