Header Ads Widget

UWT WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI,WAPANDA MITI ,WATOA ZAWADI KWA WAZAZI

Katibu wa chama cha Mapinduzi  wilaya ya Shinyanga vijijini Erenestina Richard akipanda mti kwenye kiwanja cha jumuiya ya wanawake wa chama hicho  kilichopo kata ya Iselamagazi.

Na  Kareny Masasy,Shinyanga

JUMUIYA ya umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi  (UWT) wilaya ya Shinyanga vijijini  wamesherekea  miaka 46  za kuzaliwa kwa chama hicho huku wakifanya shughuli za upandaji miti nakutembelea wodi ya wazazi katika kituo cha afya Iselamagazi.

Zoezi la upandaji miti liliongozwa na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela jana kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salum.

Ngelela pia aliongoza viongozi wa jumuiya hiyo kutembelea wodi ya wazazi  ambapo walijionea huduma zinavyotolewa kwenye kituo hicho nakuwataka watumishi waendelee kuvumilia changamoto na kutotoa lugha za matusi kwa wazazi.

Ngelela amewataka UWT kuhakikisha kiwanja ambacho wamekionyesha leo na kupandwa miti kisimamiwe na kupata hati miliki.

Aidha mganga mfawidhi wa kituo cha afya Iselamagazi dk Daniel  Singolile amesema changamoto iliyopo ni msongamano wa wagonjwa ambapo hukitumia kama  kupata rufaa kwenda hospitali ya wilaya.

Katika sherehe hizo diwani wa kata ya Iselamagazi Isack Sengerema amesema  serikali imetekeleza  ilani ya uchaguzi kwa vijiji vyote kupata huduma ya maji.

“Kata hii imepata neema kubwa kwa kupokea  zaidi ya sh Billioni tatu  katika kutekeleza miradi ya maendeleo na ujenzi wa Zahanati unakamilika kwenye kijiji cha Mwabundala”amesema diwani Sengerema.

 

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini Mecktilida Mkali akipanda mti siku walipoadhimisha miaka 46  tangu kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi
Madiwani wa  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa katika eneo la kituo cha afya Iselamagazi wakisubiri maelekezo ya kuwaona wazazi nakuwapa zawadi.
Viongozi wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini wakiongozwa na mweyekiti wa chama hicho wilaya Edward Ngelela  aliyevaa shati la kijani  wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mganga mfawidhi wa kituo cha afya Iselamagazi  ambaye hayupo pichani 
Viongozi wa chama cha Mapinduzi  wilaya ya Shinyanga vijijini wakiwa na watumishi wa  kituo cha afya Iselamagazi wakionyesha moja ya zawadi walizokuwa nazo.
Mzazi Felister Mihambo  akiwa wodi ya wazazi  kituo cha afya Iselamagazi  akipata pongezi kutoka kwa viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini pamaja na uongozi wa UWT.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela  akimpa zawadi ya sabuni mzazi Sara Richard aliyejifungua kwenye kituo cha afya Iselamagazi.
Katibu wa  UWT wilaya ya Shinyanga   vijijini akiwatambulisha  wanawake wa jumuiya hiyo kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga  Ernestina Richard  kushoto kwake ni  mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Khamis Salum akijitambulisha kwenye mkutano wa hadhara.
Katikati ni diwani wa kata ya Iselamagazi Isack Sengerema kushoto ni  mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela na kulia ni katibu wa chama hicho Ernestina Richard  wakiwa meza kuu.

 Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga vijijini Ernestina Richard akipanda mti kwenye kiwanja cha UWT kilichopo kata ya Iselamagazi.

Post a Comment

0 Comments