Header Ads Widget

VIBANDA VYA BIASHARA MANISPAA YA SHINYANGA KUTUMIWA NA WAFANYABIASHARA HALISI, SI WALIOPEWA NA KISHA KUVIPANGISHA.

 

 Mkuu wa Takukuru Mko wa Shinyaga ,Donasian Kessy akiwasilish taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 (Julai-septemba,2022) kw vyombo vya habari.

Donasian Kessy akizugumza na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga

Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakichukua kumbukumbu.

 Watumishi wa Takukuru mkoa wa Shinyanga wakifatilia taarifa ya robo ya kwaza ya mwaka wa fedha 2022/2023

Na mwandishi wetu,

TAKUKURU mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuna kuwepo na mazingira mazuri ya kufanyia baishara ili kusaidia ukuaji wa pato la Mkoa na Taifa ili kuepuka mfumuko wa bei.

Hayo yameelezwa Leo Desemba 1, 2022 na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy wakati akiwasilisha taarifa ya Takukuru kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2022(Julai-septemba, 2022) kwa vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga alisema, Takukuru kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga  walitembelea miradi ya maendeleo ili kuweza kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa ina kuwa na thamani na ubora halisi unaotakiwa kwa kuziba mianya ya rushwa  na kufanya uzuiaji rushwa kwa miradi inayotekelezwa.

Miradi 28 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 11.5  iliyotembelewa kwa kipindi cha robo ya kwanza ili kuweza kumamilika kwa ufanisi na ubora na kupelekea miradi kuwa na thamani halisi,Miradi iliyofatiliwa ni pamoja na miradi iliyotembelewa na Mwenge wa uhuru wa mwaka 2022.

Katika eneo la uzuiaji wa rushwa, Takukuru ilifanya ufatiliaji wa matumizi ya fedha katika miradi ya maendeleo ishirini na nane (28) mkoani Shinyanga ya thamani ya billion 11.5 iliyoletewa fedha na serikali, miradi iliyotembelewa ilihusu sekta ya ujenzi, elimu, maji na afya. Hii inajumuisha miradi ya Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 na fedha za tozo” Alisema Donasian Kessy

Aidha, Kessy alisema kuwa Takukuru imeendelea kushirikiana na wadau wa Halmashauri ya wilaya ya Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuna kuwepo na mazingira mazuri ya kufanyia biashara.

Mazingira hayo ni pamoja  na kupangisha vibanda vya biashara kwa wafanya biashara kwa bei nafuu na kuhakikisha vinatumiwa na wafanyabiashara halisi waliogawiwa vibanda  na siyo wafanyabiashara waliopewa vibanda  na kuwapangisha wapangaji wengine au kuuza kwa bei kubwa na kupelekea uwepo wa mazingira  magumu ya kufanyabiashara yanayoweza kuathiri pato laMkoa na Taifa na hivyo kupelekea mfumuko wa bei” Alisema Kessy,

Pia Takukuru iliweza kufanya uchambuzi wa Mfumo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala kuhusiana na changamoto za ujenzi wa madarasa kupitia fedha za UVIKO-19,

Kessy alisema , mapungufu ni pamoja na  madarasa kujengwa pasipo mkanda wa chini,wahandisi kufanya mabadiliko mbalimbali katika ujenzi wa madarasa bila kuwa na kibali kutoka mamlaka husika(RAS/OR-TAMISEMI),michoro kutofautiana kati ya halmashauri moja na nyingine na kamati za ukaguzi na upokeaji vifaa kuingiza taarifa katika vitabu kabla ya mzabuni kuwasilisha vifaa.

Mapungufu hayo yaliyobainika yatawasilishwa kwa wadau husika na kufanya kikao kuona namna ya kutatua mapungufu au mianya ya rushwa iliyobainika” Alisema Kessy.

 

Post a Comment

0 Comments