Header Ads Widget

TIMU YA MAKILAYONI YATWAA UBINGWA KOMBE LA CHEMCHEM


Timu ya Makilayoni wakikabidhiwa kombe.


Timu ya Makilayoni wakikabidhiwa kombe.
Picha ya pamoja ikipigwa

Makilayoni FC bingwa wa Chemchem CUP 2022

Mwandishi wetu, Babati

Timu ya soka ya Makilayoni FC imetwaa ubingwa wa michuano ya Chem chem CUP 2022 baada ya kuichabanga timu ya Mdori FC kwa penati 4-2 katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Mdori wilayani Babati,mkoa Manyara.


Katika mchezo huo, ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa Manyara, Makongoro Nyerere hadi dakika 90 zilipomalizika timu hizo zilitoka zimefungana 1-1.

Baada ya ushindi huo mabingwa hao ambao wametwaa mara mbili mfululizo mwaka2021 na 2022 wakipewa zawadi ya fedha taslim sh 1 milioni kombe lenye thamani ya sh 1 milioni na Mpira.

Katika michuano hiyo ambayo mwaka huu lengo lilikiwa ni kupiga vita ujangili wa Twiga jumla ya timu 16 zilishiriki kutoka katika vijiji 10 ambavyo vinaunda Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori ya Burunge(JUHIBU)

Mdori FC wakipewa zawadi ya Kombe na fedha taslim 500,000,Mpira ambapo awali timi zote 16 zilipewa seti ya jezi na mpira ili kushiriki michuano hiyo ikiwepo timi za mpira wa Pete.
Akizungumza katika michuano hiyo,Mkuu wa mkoa Manyara Makongoro Nyerere aliwataka vijana kushiriki katika kupambana na ujangili na kutunza Mazingira.

"Michezo hii sio tu ni fursa ya kukuza vipaji na kupata burudani lakini inalenga vijana kupambana na ujangili lakini pia kuhifadhi Mazingira"amesema.

Meneja mahusiano wa taasisi ya Chemchem, Charles Sylvester ambayo imewekeza shughuli za Utalii wa picha na hoteli katika eneo hilo la JUHIBU alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa miaka 10 iliyopita imekuwa na faida kubwa.

"Tumepata vipaji kuna wachezaji wametoka hapa wameenda ligi kuu lakini pia vijana wengi wamekuwa malinzi wa Wanyamapori na kupenda uhifadhi na tutaendelea kuiboresha"amesema.

Mwenyekiti wa michuano hiyo, Belela Erasto amesema michuano ya mwaka huu imegharimu zaidi ya million 50 alipongeza wawekezaji ya Chemchem kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo kila mwaka.

Erasto amesema hao waliowekeza hoteli za kitalii na Kitalu Cha Uwindaji kupitia kampuni tangu za EBN na kufanya Utalii wa picha wamekuwa na manufaa makubwa katika wilaya ya Babati na mkoa mzima wa Manyara ikiwepo kutoa ajira zaidi ya 300 ,ujenzi wa shule,kusaidia sekta ya afya,maji na vikundi vya wanawake.

Post a Comment

0 Comments