Header Ads Widget

MZEE WA MIAKA 62 APANDISHWA KIZIMBANI TUHUMA KUMBAKA MWANAFUNZI DARASA LA SITA
Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani, Maxmilian Malima (62) amepandishwa kizimbani akikabiliwa na tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Kilangalanga mkoani humo.

Akisoma maelezo ya awali leo Jumanne Desemba 13, 2022 mwendesha mashtaka wa Serikali, Rose Ishabakaki akisaidiana na Eliza Olomi mbele ya hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Fahamu Kibona amesema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo kwa nyakati tofauti tofauti mwezi Julai na Octoba 2022.


Amesema kuwa siku moja kati ya mfululuzo wa matukio hayo mtuhumiwa huyo alimuita Mwanafunzi huyo wakati akielekea shuleni na kumtuma dukani akamnununulie mahitaji na aliporejea alimvutia ndani ya nyumba yake kísha kumfanyia kitendo hicho.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANACHI.

Post a Comment

0 Comments