Header Ads Widget

SHIVYAWATA WAOMBA MIUNDOMBINU YA UMEME MABWENI KITUO JUMUISHI CHA WALEMAVU BUHANGIJA ICHUNGUZWE

Shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga  (Shivyawata) limeomba serikali kufanya uchunguzi wa mifumo ya umeme katika miundombinu ya mabweni  kituo jumuishi  cha watoto wenye ulemavu Buhangija.
 
Salvatory  Ntandu  Shinyanga

Shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga (SHIVYAWATA) limeiomba serikali kufanya ukaguzi wa mifumo ya miundombinu ya umeme katika mabweni ya shule ya Msingi Bungangija mchanganyiko ili kudhibiti majanga ya moto.

Ombi hili limetolewa na Mwenyekiti wa SHIVYAWATA mkoa  wa Shinyanga Gerald Mpongo katika zoezi la kuaga miili ya wanafunzi watatu walipoteza maisha Novemba 24 mwaka huu baada ya kuungua moto bweni walilokuwa wamelala katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo.

Amesema kuwa ipo haja kwa serikali kuhakiki mifumo ya umeme katika mabweni na madarasa ya majengo ya shule hiyo ambayo yalijengwa muda mrefu ili kukabiliana na majanga kama vile moto ambao umesababisha wanafunzi watatu wenye ulemavu wa macho kupoteza maisha wakiwa wamelala.

“Serikali kupitia shirika la umeme Tanzania (Tanesco ) mkoa wanatakiwa kukagua mifumo hiyo ikiwezekana kuibadilisha kwani iliyopo imeshachakaa kutokana na kuwekwa muda mrefu,na itasaidia kuongeza ufanisi wa kuzuia majanga ambayo yanaweza kuzuilika,”amesema Mpongo.

Sambamba na hilo Mpongo aliomba serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo, ili wazazi na walezi wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho wasieendelee kuwa na hofu juu ya usalama wa watoto wao katika kituo hicho.

Kwa upande wake Shekh wa wilaya ya Shinyanga Sudi Katengire aliwaomba wazazi na walezi kuwa watulivu wakati serikali ikielendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuwaomba kuendelea kuwaombe kwa Mungu watoto waliotangulia mbele za haki.

Awali akitoa salamu za serikali  mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema alisema kuwa tayari serikali imekwisha chukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kumwagiza mkuu wa jeshi na zimamoto kuhakikisha wnafanya uchunuzi wa tukio hilo pamoja na kutoa elimu ya kukabiliana na majanga kwa wanafunzi.

“Serikali imegharamia mazishi ya wanafunzi hawa,tunatoa pole kwa wazazi waliowapoteza watoto wao kuhusiana na janga la moto ,sisi kama serikali tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili ili kubaini  chanzo chake niwaombe muwe watulivu,”amesema Mjema.

Mwenyekiti wa Shivyawata mkoa wa Shinyanga Richard Mpongo akielezea namna walivyoguswa na msiba huo.

Post a Comment

0 Comments