Header Ads Widget

SAUTI YA MAMA YAWAPA ELIMU YA UKATILI WANAFUNZI SHULENI

Baadhi ya wanakikundi cha Sauti ya mama ambao ni wasanii wa filamu
              Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wanakikundi cha Sauti ya mama ofisini kwake.

Jamii imetakiwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana na kuishi nao kwenye jamii ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa ni changamoto kubwa kwenye jamii na kusababisha baadhi ya watoto kushindwa kupata elimu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kikundi cha Sauti ya Mama kutoka Jijini Dar es salam Samila Rashid ambao ni wasanii wa filamu wakati wakitoa elimu ya ukatili wa kijinsia  juu ya kupinga mimba na ndoa za utotoni pamoja na elimu kwa vijana kwenye shule za msingi na sekondari Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na taasisi ya Holy Smile yenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Sauti ya mama amesema kuporomoka kwa maadili katika jamii ni chanzo cha matukio mengi ya ukatili wa kijijinsia kwa watoto vikiwemo vitendo vya ubakaji na kulawiti hali ambayo inatakiwa kukemewa vikali na wadau wa kupinga ukatili,jamii na serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Holy smile Arnold Bweichum amesema katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia wameamuwa kushirikiana na Sauti ya mama kutoa elimu mashuleni juu ya kupinga vitendo hivyo.

Amesema wametoa elimu katika shule tano za Mkoa wa Shinyanga ili kuwawezesha wanafunzi kutambua athari za ukatili wa kijinsia na kujua namna ya kujiepusha na vitendo hivyo ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo yao.

Amesema kampeni hiyo ya kutoa elimu mashuleni ni mwendeleo ili kuhakikisha watoto na jamii nzima inapata uelewa. 

Mwenyekiti wa Kikundi cha Sauti ya mama Samila Rashid akizungumza na wanafunzi juu ya suala zima la ukatili wa kijinsia.
                Sauti ya mama wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine
            Mkurugenzi wa Taasisi ya Holy Smile Arnold Bweichum akieleza lengo la kutoa elimu mashuleni


            Elimu ikiendelea kutolewa 

Afisa vijana Manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula akizungumza na wanafunzi
     
                          wakiwa kwenye kikao na wanafunzi
        Wanafunzi wakiwasikiliza wataalamu

wakipatiwa elimu

             



 

Post a Comment

0 Comments