Header Ads Widget

TAWASANET YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA


Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Na Marco Maduhu, DODOMA

TANZANIA Water and Sanitation Network (TAWASANET), wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari, kutambua masuala yanayohusu Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira, ili wanapokuwa wakiandika habari zao waandike kwa ufasaha.

Mafunzo hayo yametolewa siku mbili Jijini Dodoma, kuanzia Novemba 16, 2022  na yamehitimishwa leo Novemba 17, yakifadhiliwa na Taasisi ya Foundation For Civil Society.

Mratibu wa Mradi wa (TAWASANET) Darius Mhawi, amesema mafunzo hayo yamehusisha vyombo mbalimbali vya habari kutoka Mikoa ya Dar es Salam, Dodoma, Ruvuma, Mwanza na Shinyanga, wakiwamo wa Magazeti, Radio na Television, ambao watatumia kalamu zao kuandika habari kwa wingi zinazohusu maji na usafi wa mazingira.

“Sekta ya maji ni nyeti sana inaguza maisha ya kila siku ya mwanadamu, hivyo waandishi wa habari wakiielewa vizuri watakuwa wakiandika habari zao kwa usahihi, ikiwamo kuelimisha, kuonya na kukosoa, na hatimaye kila kitu kwenda sawa,”anasema Mhawi

Nao Waandishi hao wa habari wamesema mafunzo hayo yamewaongezea ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao katika kuandika habari za maji na usafi wa mazingira.

Mratibu wa Mradi wa (TAWASANET) Darius Mhawi, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Mratibu wa Mradi wa (TAWASANET) Darius Mhawi, akiendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Mwezeshaji Severine Allute akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Mwezeshaji Severine Allute akiendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Post a Comment

0 Comments