Header Ads Widget

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOPITISHWA KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA

 
Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Na Mwandishi Wetu , SHINYANGA

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, ametaja majina ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti mkoani humo, ambayo yamepitishwa na Halmashauri kuu ya CCM Taifa.

Akizungumza kwa njia ya simu akitokea Dodoma, amewataja waliopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga kuwa ni Mabala Mlolwa ambaye anatetea kiti chake kwa awamu nyingine tena, Mwingine ni Costantine Mollo Nkuba, Eneza Onel Kanuya.

Nafasi ya ujumbe wa wa halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC) waliopitishwa ni Gasper Hanson Kileo ambaye anatetea nafasi yake kwa mara nyngine, mwingine ni Nyachiro Maiga Magongo na Majuto Clement Manyilizu.

Post a Comment

0 Comments