Header Ads Widget

MADIWANI KISHAPU WAMEIOMBA SERIKALI KUONGEZA USAMBAZAJI WA MBEGU ZA PAMBA KWA WAKULIMA

Madiwani wa Halimashauri ya wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha baraza.

Baraza la madiwani wilayani Kishapu likiendelea.

Baraza la madiwani wilayani Kishapu likiendelea.

Baraza la madiwani wilayani Kishapu likiendelea.

Na Halima Khoya, KISHAPU

MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, wameiomba Serikali kuongeza usambazaji wa mbegu za Pamba kwa wakulima wilayani humo.  
Wamebainisha hayo leo Novemba 2, 2022 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wilayani Kishapu.

Wamesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya uchache wa mbegu za Pamba kwa wakulima wilayani humo, ambao umesababishwa na wadudu kula mbegu hizo mashambani.

"Tangu tuanze kupanda pamba kumekua na changamoto ya uchache wa mbegu unaosababishwa na kuanzishwa kwa mbinu mpya ya kupanda pamba kwa kuchimba mashimo ambapo wadudu wanakuja kula mbegu hizo mashambani na kusababisha upungufu wa mbegu kwa wakulima,” amesema Michael Paulo diwani wa Shangihilu.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, ameahidi kulifanyia kazi suala hilo la usambazaji wa mbegu za kutosha kwa wakulima, hali ambayo itaongeza uzalishaji na halmashauri kupata mapato mengi ya kutosha.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, amewataka pia wananchi wilayani humo wajikite kwenye kilimo cha mazao ambayo yanastahimili ukame ili kuendana na mabadiliko ya tabia nchi.

Post a Comment

0 Comments