Header Ads Widget

THOMAS MUYONGA ACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KAHAMA


Mshindi wa kiti cha uenyekiti wilaya ya Kahama kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Thomas Muyonga  akiwashukuru wajumbe  baada ya kumchagua kwa kura nyingi.

Na Kareny  Masasy, Kahama

THOMAS Muyonga  ameshinda nafasi ya  mwenyekiti  wilaya ya Kahama kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 1,722 dhidi ya  wapinzani wake Costantine  Makoye aliyepata kura  179 na  Michael Kulwa aliyepata kura 127.

Uchaguzi huo ulianza jana tarehe 1 mwezi October  na kukamilika leo tarehe 2  mwezi October mwaka 2022   kwa kuendelea   kuchagua  kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya wilaya huku wajumbe takribani  2028 walijitokeza kupiga kura kwa nafasi ya mwenyekiti wilaya.

Msimamizi wa uchaguzi huo  James Kusekwa ametangaza  matokea na majina ya waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali ambapo  alimtangaza mwenyekiti Thomas Muyonga kuwa mwenyekiti wa CCM wilaya baada ya  kutetea kiti hicho kwa awamu ya pili  sasa.

Kusekwa  amemtangaza  katibu  wa siasa  itikadi na uenezi   Joackim  Simbila  aliyetetea kiti hicho  kwa kupata kura  151 dhidi ya wapinzani wake Mola Zabron aliyepata kura  72  na Ambrose Nkwabi aliyepata  kura 44 huku wajumbe waliopiga kura kwenye nafasi hiyo  wakiwa 267.

Aidha Kusekwa aliendelea kutangaza makundi ya uwakilishi ambapo kundi la vijana mshindi alikuwa Godfrida Simba  aliyepata kura 261 kati ya kura 263, kundi la wazazi  Julias Lugobi aliyepata kura  203 huku kundi la uwakilishi  umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi  (UWT)  alichaguliwa Juliana  Kajala.

Baada ya kutangwa kwa matokeo hayo  mshindi  Thomas Muyonga alipata nafasi  ya kuwasalimia wajumbe nakueleza kuwa uchaguzi umekwisha wanatakiwa wasonge mbele kazi iendelee na kuvunja makundi yaliyokuwepo.

Muyonga amewashukuru wajumbe kwa kuwa wavumilivu kwa zoezi la uchaguzi lililoanza jana  na kumchagua kuendelea kuongoza kiti hicho kwa kipindi cha miaka mitano tena.

Wajumbe wakiwa ukumbini wakisubiri maelekezo.
Wajumbe wakiwa ukumbini

Uchaguzi  wilayani Kahama.

Wajumbe  wa mkutano mkuu wa wilaya walipokuwa kwenye uchaguzi.

Mwenyekiti wa Thomas Muyonga akiwa meza kuu na msimamizi wa uchaguzi  James Kusekwa.

Mwenyekiti   Thomasi Muyonga baada ya kuchaguliwa na kushinda akisumbiri matokeo ya kamati ya utekelezaji  

Wajumbe wakimbeba katibu wa siasa   itikadi na uenezi Joackim Simbila baada ya kutangazwa mshindi.

Wajumbe wakimbeba katibu  wa siasa itikadi na uenezi wilayani Kahama Joackimu Simbila 


Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Kahama  baada ya ushindi akiongea  kwa kuwashukuru wajumbe kumchagua tena kwa awamu ya pili.

Post a Comment

0 Comments