Header Ads Widget

SHINYANGA WAJIVUNIA MAFANIKIO SEKTA YA AFYA AWAMU YA SITA, HOSPITALI MPYA YA RUFAA MWAWAZA YAANZA KUTOA MATIBABU RASMI


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKOA wa Shinyanga umeelezea mafaniko makubwa katika sekta ya afya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha huduma za afya mkoani humo hadi kufikia hatua ya kuhamia rasmi katika Hospitali mpya ya Rufaa iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu ameelezea mafanikio hayo leo Septemba 8, 2022 wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia, imefanya mambo makubwa katika Sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu, ikiwamo na ujenzi wa Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.

“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za Afya hapa nchini ukiwamo na Mkoa wa Shinyanga, ambapo tumepata fedha nyingi na tumejenga majengo mengi yakiwamo ya huduma ya dharura, mlipuko wa Magonjwa, Wagonjwa Mahututi, pamoja na jengo la kuzalisha hewa ya Oksijeni,”amesema Mulyutu.

Aidha, amesema pia katika kuboresha huduma hizo za afya mkoa wa Shinyanga umefikia hatua ya kuhamia rasmi kwenye Hospitali yake mpya ya Rufaa mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga na huduma zimeanza kutolewa, na kumpongeza Rais Samia kwa kuijali Sekta ya Afya na kuimarisha Afya za wananchi.

Post a Comment

0 Comments