Header Ads Widget

HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MSALALA IMEANZA KUTOA HUDUMA,WANANCHI WASHUKURU KUOKOA SAFARI ZA MBALI KUFUATA MATIBABU

Hospitali ya halmashauri ya  Msalala  wilayani Kahama mkoani Shinyanga imekamilika ujenzi wake  nakupata watumishi wa afya sasa imeanza kufanya kazi.

Na Kareny  Masasy, Msalala

HOSPITALI ya halmashauri ya  Msalala imeanza kutoa baadhi ya  huduma  ikiwemo kliniki ya mama na mtoto na wagonjwa wa nje (OPD)  ili kuwaepusha na kusafiri umbali mrefu kupata huduma.

Mganga mkuu wa  halmashauri hiyo dkt Ernest Chacha  amesema hayo jana hospitalini hapo  nakueleza kuwa  ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu  sh Billioni 1.8  nakuwanufaisha wakazi takribani 500,000.

 Dkt Chacha amesema kuwa hospitali hiyo  kuna jengo la wagonjwa wa nje  (OPD) Maabara,ICU,Mama na mtoto famasi, chumba cha kuhifadhia maiti, chumba cha kuchomea taka pamoja na nyumba ya mtumishi.

“Kuanza kufanya kazi hospitali hii kutapunguza safari za wagonjwa  na wajawazito wanaopewa rufaa kwenda manispaa ya Kahama kutoka kwenye Zahanati 36 zilizopo kwenye halmashauri hii watatibiwa hapahapa”amesema  dkt Chacha.

Dkt Chacha amesema  kuwa  Kuna   watumishi  wa afya 57  na katika hospitali hiyo  wamepata watumishi  wa afya 18 na fedha za vifaa tiba na dawa kiasi cha sh Millioni 376  .

“Changamoto iliyopo ni uhaba wa maji kwenye hospitali hiyo  kutokana na kukosekana kwa chanzo cha  uhakika   kwani ninaiomba serikali kuharakisha  mradi wa maji wa Nduku - Busangi chanzo ”amesema dkt Chacha..

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo  dkt Fredrick Macha amesema kuwa huduma zilikuwa ni ngumu kutokana na uhaba  wa vifaa tiba  lakini sasa mashine za mionzi zipo  watumishi wapo wakutumia vifaa vilivyopo.

“ Hospitali hii imekamilika kilichosababisha kutoa huduma baadhi ni changamoto ya  uhaba wa maji kwani daktari wa upasuaji wapo,chumba cha kujifungulia  na wauguzi  wapo” amesema dkt Macha.

Diwani wa kata ya Ntobo iliyopo hospitali hiyo  David Mlyandali amesema kuwa  hospitali kuanza kutoa huduma wamefarijika sana wananchi  walikuwa wakitumia gharama kubwa kumsafirisha mgonjwa.

Mlyandali amesema kuwa  changamoto ya ukosefu wa maji  serikali imeanza kulifanyia kazi licha ya hospitali pia  wananchi nao wamekuwa wakiteseka  kwa kununua maji au kutumia maji ya visima vifupi.

Wakazi wa halmashauri ya Msalala Tabu Embasi  na Clement Mihayo  waliofika kupata huduma za afya katika hospitali hiyo wamesema kuwa kuanza kwa hospitali hiyo kumesaidia   kwani  wajawazito na wagonjwa wengine walikuwa wakipoteza maisha njiani kutokana na barabara  kuwa mbovu na umbali kwenda manispaa Kahama.

 

Post a Comment

0 Comments