Header Ads Widget

DC KISWAGA ATAKA MAAFISA UTUMISHI WAFUATE MAELEKEZO JUU YA KUPANDISHA WALIMU MADARAJA NA KUFUATILIA WANAOKARIBIA KUSTAAFU




MKUU wa wilaya ya Kahama  Festo Kiswaga akizungumza kwenye  mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania CWT wilayani Kahama mkoani Shinyanga 

Na  Kareny  Masasy,  Kahama

Mkuu  wa wilaya ya Kahama   mkoani Shinyanga Festo Kiswaga  ametoa maelekezo kwa  maafisa utumishi wa halmashauri   kuhakikisha wanafuata utaratibu wa kuwahisha  taarifa za watumishi wanaokaribia kustaafu na wale wanaotarajia kupanda madaraja kazini  ili kuondoa ucheleweshaji wa stahiki zao.

Kiswaga amesema hayo  leo tarehe 23/09/2022  alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ulio wakutanisha wajumbe takribani 250.

Kiswaga amesema amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya ingawa kulikuwa na changamoto ya mazingira ya kuishi wa walimu serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imeanza kuyafanyia kazi na hata waliopandishwa madaraja  wanalipwa stahiki zao .

Kiswaga amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imetekeleza kwa kiasi kikubwa matakwa ya walimu na kutoa maelekezo  ikiwa  maafisa utumishi wanatakiwa  kuangalia wale wote wenye kukaribia kustaafu  kuwaandalia nyaraka zao mapema ili kuondoa kero.

“Nimeambiwa kuna watu  ambao wako halmashauri ambao wamekuwa wakichelewesha  kuwapandisha madaraja walimu sasa tunashughulika nao nakuchunguza kwanini wanachelewesha nanyi walimu mkiwa na shida  msikae kwenye mabenchi kusubiri bali mpite moja kwa moja msikilizwe  muwahi  kufundisha wanafunzi wetu”amesema Kiswaga.

Mwenyekiti wa  CWT mkoa wa Shinyanga  Mathias   Balele amesema  kuwa serikali imefanya kazi kubwa kwa walimu kwani imeweza kuwajengea nyumba na mazingira ya kufundishia kuwa mazuri huku upandishaji wa madaraja ukienda vizuri tofauti na zamani.

Mwenyekiti wa  CWT wilaya ya Kahama  Raymond Lutemba  akiongoza mkutano huo kupitia taarifa ya utendaji kazi kwa chama hicho kwa kipindi cha miaka miwili na nusu (March 2020 – Septemba 2022) nakueleza kero mbalimbali wamezitatua ikiwemo uhamisho wa walimu na wale bado mazungumzo  yanaendelea na waajiri wao.

 Pia kulikuwa na  ajenda ya  kuondokana na usafiri wa gari aina ya Coaster iliyokuwa ikibeba abira 25  hali ambayo walieleza inawapa changamoto katika suala la usafirishaji  na kuwa bovu mara kwa mara.

Ambapo wajumbe wa mkutano huo walipendekeza kununuliwe gari aina ya TATA itakayobeba abiria 40  itakayosaidia katika kuwasafirisha wao wanapokuwa na shughuli mbalimbali .

Wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakisimama tayari kumpokea mgeni rasmi katika mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama wakiwa katika sala kabla ya mkutano kuanza

Wageni waalikwa katika mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama wakiwa meza kuu
Katibu  CWT wilaya ya Kahama  Peter Gedi akitoa utangulizi katika mkutano mkuu wa chama hicho.
Mweyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga Mathias Balele akisalimiana na wajumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Kahama


Wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga



Wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga

wageni waalikwa wakiwa meza kuu ni mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga kushoto katikati ni Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga Mathias Balele na upande wa kushoto ni kaimu katibu wa CWT mkoa wa Shinyanga Allen Shuri
Wajumbe wa kamati tendaji ya CWT mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Kahama Raymond Lutemba akiongea kwenye mkutano
Katibu wa CWT halmashauri ya Ushetu Alponnce Mbasa mgeni mwalikwa akisalimia wajumbe wa mkutano mkuu




Mwenyekiti wa CWT halmashauri ya Ushetu akisalimiana na wajumbe wa mkutano mkuu alipoalikwa CWT wilaya ya Kahama.

DK Baraka  .C ,Kulwa  Mkurugenzi  wa   hospitali ya CKM  iliyopo Runzewe  wilaya ya Bukombe mkoani Geita  akiwa mdau wa elimu akihudhuria mkutano mkuu  kwa kutoa salamu zake.

Post a Comment

0 Comments