Header Ads Widget

SHIRIKA LA CORDS LAJENGA DARASA LA MEMKWA

Shirika la CORDS lajenga Darasa la MEMKWA
Darasa la Memkwa.
Ndani ya darasa la Memkwa.
 
Picha ya pamoja ikipigwa mbele ya darasa la Memkwa.
 
Mwandishi wetu,longido

Taasisi ya Utafiti,Maendeleo na Huduma kwa jamii(CORDS) jana imekabidhi darasa lililojengwa maalum kwa Vijana wa jamii ya Kimasai wa kike na kiume ,ambao wamekosa fursa ya kusoma katika mfumo rasmi shule ya Msingi(MEMKWA).

Darasa hilo limegharimu kiasi cha sh 33.5 milioni lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 45 na litakuwa katika shule ya msingi Ngoswak iliyopo kata ya Engareinabor wilaya ya Longido mkoani Arusha na limejengwa na shirika hilo la CORDS


Akizungumza wakati wa kukabidhiwa darasa hilo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Longido, Simon Laizer alishukuru shirika la CORDSna wafadhili shirika la Douglas Scott Foundation la nchini Australia kupitia mradi wa action on poverty. kujenga darasa hilo.

"Darasa hili litasaidia sana vijana ambao hawakusoma katika mfumo rasmi wake hapa kusoma na hivi kupambana na ujinga na umasikini"alisema

Mkurugenzi wa shirika la CORDS
Lilian Looloitai alisema darasa hilo litakuwa fursa ya pekee kuwasaidia watoto husuani wa kike ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na shule kwa wakati.

Alisema kuwa mazingira ya jamii za pembezoni hususani wafugaji wa kimasai zinazokabiliwa na changamoto nyingi ambazo hupelekea watoto kutopata nafasi ya kuanza masomo kutokana na kukosekana madarasa maalum ya Memkwa ambayo huwapelekea kutokuwa na ari ya kuanza kusoma masomo hayo ya elimu ya msingi.

Amesema mwaka 2019 na 2020 walikuwa na mradi wa kuandikisha wanafunzi wa Memkwa wapatao 20 na kuanza kufundishwa shuleni hapo lakini kutokana na kukosa chumba maakum cha kuwafundishia walipelekwa shule ya msingi.

Mkurugenzi wa shirika la Douglas Scott foundation toka Australia,Adrian Scott amesema kuwa wanafurahi kusaidia ujenzi wa darasa hili kwani litasaidia kuondoa ujinga kwa watoto na pia kuwezesha kujikwamua kiuchumi

Naye mkuu wa shule hiyo Kwamboka Nyanami Phirace amewashukuru Cords kwa kuwajengea darasa hilo na kuahidi kushirikiana na uongozi wa kijiji kuhamasisha wazazi kuandikisha wanafunzi wa kutosha darasa hilo na wataanza masomo yao rasmi January 2023.

Post a Comment

0 Comments