Header Ads Widget

TRA KUTOA ELIMU YA MLIPA KODI MLANGO KWA MLANGO, RC MJEMA ATIA NENO KWA WAFANYABIASHARA MKOANI SHINYANGA

TRA KUTOA ELIMU YA MLIPA KODI MLANGO KWA MLANGO
Afisa Mkuu msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Edwin Iwato, (kushoto) akimkabidhi Zawadi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) imeanza kampeni ya kutoa elimu kwa mlipa Kodi kwa wafanyabiashara mkoani Shinyanga, ambayo itafanyika mlango kwa mlango, ili kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari.

Afisa Mkuu msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Edwin Iwato, amebainisha hayo June 3, 2022 mkoani Shinyanga wakati wakitambulisha kampeni hiyo ya elimu kwa mlipa Kodi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Amesema dira ya TRA ni kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani, na kuwataka wafanyabiashara wawe wazalendo na nchi yao na kulipa Kodi kwa hiari yao wenyewe, bila kutumia mabavu.

"Kampeni hii ya elimu ya mlipa kodi inayo julikana Amsha Amsha Kampeni, tutaitoa ndani ya mwezi mzima hapa mkoani Shinyanga, kwa kutembelea wafanyabiashara wote mlango kwa mlango na kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari," amesema Iwato.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ametoa wito kwa wafanyabiashara mkoani Shinyanga wajenge utamaduni wa kulipa kodi hiari, ili Serikali ipate fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha, Mjema amewasihi pia wafanyabiashara wawe waaminifu, kuwa wanapouza bidhaa zao watoe Risiti, pamoja na wananchi wakinunua wadai Risiti, jambo ambalo litafanikisha Serikali kufikia malengo yake ya ukusanyaji mapato.

Katika hatua nyingine Mjema ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi wa mkoa huo wa Shinyanga, kuwa siku ya zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi Agost 23 mwaka huu, wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa, ili Serikali ipate idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo.

Alisema Serikali ikiwa na idadi ya watu wake, itakuwa virahisi kupanga mikakati yake na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo kulingana na uhitaji wao, na kuwasihi siku hiyo wabaki majumbani ili wahesabiwe.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye utambulisho wa uzinduzi wa Amsha Amsha Kampeni ambayo itafanywa na TRA kutoa elimu ya mlipa Kodi mkoani humo.

Afisa Mkuu msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Edwin Iwato, akielezea madhumuni ya Amsha Amsha kampeni ya utoaji elimu ya mlipa Kodi.

Mkutano wa TRA wa Amsha Amsha kampeni ukiendelea kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Afisa Mkuu msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Edwin Iwato, (kushoto) akimkabidhi Zawadi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Maofisa wa TRA wakipiga picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (watatu kutoka kulia),
 
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments