Header Ads Widget

JELA MIAKA 31 KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

Mahakama  ya Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga, imemhukumu kwenda jela miaka 31 mkazi wa mji wa Handeni Wilaya humo, Ibrahim Mgaza kwa makosa matatu, likiwamo la kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, John Chacha alisema licha ya utetezi wa mshtakiwa, mahakama hiyo imemtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 31.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Chacha alisema mshitakiwa alitenda kosa la kubaka kinyume na kifungu cha 130 (1), (2) (e) na 131(1) cha sheria ya adhabu ya makosa ya jinai sura ya 16 R.E 2019 na kosa la pili, ni la kumpa ujauzito mwanafunzi kinyume cha kifunga 60.A (3) cha sheria ya elimu kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria na 2/2016.

Hakimu huyo alisema kosa la tatu, ni la kumtorosha mwanafunzi kutoka kwa wazazi wake kinyume na kifungu cha 134 na 35 cha sheria ya adhabu ya makosa ya jinai sura ya 16 marejeo ya mwaka 2019.

SOMA ZAIDI HAPA-Chanzo Mwananchi

Post a Comment

0 Comments