Header Ads Widget

CHANZO CHA AJALI BASI LA ZUBERI KUUWA WATU WATATU SHINYANGA


 Basi la Zuberi likiwa limepata ajali

Na Marco Maduhu.

Watu watatu wamefariki dunia saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya Safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga George Kyando, amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano June 15, 2022 majira ya saa nane mchana katika barabara ya Mwanza Shinyanga ambapo basi hilo lenye namba za usajili T435 DJS SCANIA liligonga ukingo wa daraja la Mwigumbi na kutumbukia bondeni.

Kamanda Kyando ametaja mmoja wa waliofariki dunia kuwa ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Haule.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva alipata tatizo la kiafya akiwa safarini.

Aidha, ametoa wito kwa madereva kuchunguza afya zao kabla ya kuanza safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Post a Comment

0 Comments