Header Ads Widget

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU ATAJA SABABU ZA KUWATUMBUA WAKURUGENZI WATANO MSD

Wakurugenzi watano MSD waondolewa


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametangaza kuondolewa kazini Wakurugenzi watano wa Bohari ya Dawa (MSD), kufuatilia malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na wabunge na wadau wengine kuhusu utendaji usioridhisha wa bohari hiyo.

Waziri Ummy Mwalimu ameliambia bunge jijini Dodoma kuwa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kubadilisha uongozi wa juu wa MSD na kumteua mwenyekiti mpya wa bodi, hatua hiyo ilikuwa haitoshi kutokana na malalamiko mengi yaliyokuwa yakitolewa.

“Mkurugenzi wa Fedha anaondoka MSD, Mkurugenzi wa manunuzi MSD, Mkurugenzi wa Logistics MSD, Mkurugenzi wa Sheria MSD na Mkurugenzi wa Utawala wa MSD anaondoka.” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Waziri huyo wa Afya ametangaza uamuzi huo wakati akihitimisha mjadala wa bajeti kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, baada ya kuchangiwa na wabunge mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments