Header Ads Widget

MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA KWA WANAHABARI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO YAHITIMISHWA DODOMAMkufunzi wa masuala ya ulinzi wa mitandao (Digital Security) Mussa Juma akitoa mafunzo ya usalama na matumizi ya mitandao kwa waandishi wa habari katika utekelezaji wa majukumu yao.

Na Marco Maduhu, DODOMA

MAFUNZO ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari na matumizi sahihi ya mitandao katika utekelezaji wa majukumu yao, yamehitishwa Rasmi Jijini Dodoma kwa kushirikisha waandishi wa habari 20 kutoka Mikoa mbalimbali hapa nchini, ili kuwa salama katika utendaji wao kazi.

Mafunzo hayo yalianza jana Mei 30, 2022 na kuhitimishwa leo Mei 31, ambayo yameendeshwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Shirika la International Media Support.

Mratibu wa mafunzo kutoka (UTPC) Victor Maleko, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaweka katika hali ya usalama waandishi wa habari, katika utekelezaji wa majukumu yao na matumizi sahihi ya mitandao.

“Mafunzo haya tunayatoa kwa waandishi wa habari 100 na sasa tumeshatoa kwa waandishi 80, na mafunzo ya mwisho ya waandishi wa habari 20 waliosalia yatafanyika Jijini Mwanza,”amesema Maleko.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Mussa Juma, amewataka waandishi wa habari hapa nchini, wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao, wazingatie kwanza usalama wao, kufuata maadili ya uandishi wa habari pamoja na kuwa makini na matumizi ya mitandao ili kuendelea kuwa salama.

“Unapotaka kwenda kukusanya taarifa hasa katika maeneo ambayo ni hatari, soma kwanza mazingira ya eneo husika kuona kama usalama wako upo, sababu maisha yako ni zaidi ya habari, pia msiweke picha hovyo mitandaoni (Post) kuonyesha mahari ulipo ni hatari sana katika usalama wako,”amesema Juma.

Nao Waandishi wa habari wamefurahia mafunzo hayo, na kubainisha kuwa yametolewa katika muda muafaka, ikiwa kwa sasa dunia ipo kwenye ulimwengu wa Teknolojia na ni muhimu kwa waandishi wa habari kuwa makini na matumizi ya mitandao ili kuwa salama katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mkufunzi Mussa Juma akitoa mafunzo ya usalama kwa waandishi wa habari na matumizi sahihi ya mitandao.

Mussa Juma akiendelea kutoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari.

Mratibu wa Mafunzo kutoka Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Victor Maleko akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya ulinzi na usalama katika utekelezaji wa majukumu yao na matumizi sahihi ya mitandao.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya mafunzo hayo kuhitimishwa.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya mafunzo hayo kuhitimishwa.

Na Marco Maduhu, DODOMA.

Post a Comment

0 Comments