Header Ads Widget

WAZIRI JAFO, WENZAKE WATATU KIKAANGONI BUNGENI WIKI HII

Waziri Jafo, wenzake watatu kikaangoni bungeni wiki hii

Wakati Bunge la Bajeti likitarajia kuendelea na vikao vyake kesho, wiki hii mawaziri watatu wanatarajiwa kuwekwa kikaangoni pale watakapowasilisha makadirio na matumizi ya wizara zao kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Hata hivyo, macho na masikio ya Watanzania, yataelekezwa kwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) inayoongozwa na Dk Selemani Jafo, ambaye atalazimika kujibu hoja za wabunge kutokana na mambo kadhaa yaliyojitokeza nchini.

Kwa miaka ya nyuma hoja kubwa katika wizara hiyo zilitawaliwa na masuala ya Muungano, lakini safari hii kuna uwezekano mkubwa kuibuka suala la mazingira, hasa uchafuzi wa Mto Mara.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments