Header Ads Widget

WABUNGE WAIKATAA RIPOTI YA MTO MARA

. Wabunge leo Jumanne Aprili 5, 2022 wameikataa ripoti ya uchunguzi wa uchafuzi wa maji na vifo katika mto Mara wakisema ni ya aibu na inaifedhehesha nch
Ripoti hiyo ni ile iliyofanya uchunguzi wa uchafuzi wa maji kuwa na rangi nyeusi na kusababisha vifo vya samaki katika mto mara ambayo ilikuwa chini ya Profesa Samweli Mayele na wajumbe wengine 10.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Seleman Jafo aliunda kamati kuchunguza chanzo cha tatizo hilo lakini baada ya kuwasilishwa kwa wananchi ilizua mjadala karibu kila kona.

Kinyesi cha mifugo chatajwa kuwa chanzo cha kufa samaki mto Mara

Leo, wabunge 18 wote wameipinga ripoti hiyo na kuomba isiwekwe kwenye mtandao maalumu wa serikali kwa kuwa maelezo yake ni ya aibu.

Baada ya kamati hiyo kumaliza kuwasilisha ripoti hiyo mbele ya wabunge, mbunge wa Viti Maalumu Neema Rugangira alifungua pazia la kuchangia na alitaja chanzo cha kuwa na taarifa mbovu ni kwa sababu baadhi ya wajumbe wake wana maslahi binafsi. Advertisement


Rugangira pia alihoji kama uchunguzi ulikuwa unahusisha mambo ya vyakula, kwa nini Wizara ya Afya na Shirika la Viwango (TBS) hawakushirikishwa.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments