Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI KATAMBI AAHIDI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WATU WENYE ULEMAVU

NAIBU WAZIRI KATAMBI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATU WENYE ULEMAVU

Picha; Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi, (wapili kulia) akila chakula na watu wenye ulemavu Dodoma jana kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge Shinyanga mjini Patrobas Katambi, ameahidi kuendela kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.
 
Katambi alibainisha hayo Aprili 17, 2022 wakati akila chakula cha pamoja na watu wenye ulemavu katika kituo cha Samaria kilichopo Kata ya Hombolo Jijini Dodoma wakati akisherehekea nao sikukuu ya Pasaka.

Kituo cha Samaria kilichopo kata ya Hombolo ni moja ya kituo kinachotoa huduma kwa watu wenye ulemavu,wazee, wenye ukoma na ugonjwa wa macho.

Hata hivyo mhe. Katambi ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuwapunguzia changamoto za kimaisha,miundombinu kama sehemu ya idara katika Wizara yake

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi, (wapili kulia) akila chakula na watu wenye ulemavu Dodoma jana kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi, (kulia) akipakua chakula kusherehekea sikukuu ya Pasaka na watu wenye ulemavu.

Post a Comment

0 Comments