Header Ads Widget

BABA AUAWA KWA MADAI YA KUFUMANIWA AKIWA AMELALA NA MKE WA MTOTO WAKE KITANDANI

Baba auawa kwa madai ya kufumaniwa akiwa amelala na mke wa mtoto wake kitandani


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, linamshikilia kijana Mwandu Shija (32) mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga, kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Shija Robert (55) kwa madai ya kumfuma akiwa amelala na mkewake kitandani.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akitoa taarifa leo kwa vyombo vya habari, alisema tukio hilo limetokea jana majira saa 8 usiku, wakati kijana huyo aliporudi nyumbani ndipo akamfuma baba yake akiwa amelala na mkewake na kuanza kumshambulia.

Alisema wakati kijana huyo akiendelea kumshambulia Baba yake na kipande cha kuni sehemu mbalimbali za mwili wake, ndipo alipompiga sehemu mbaya na kusababisha mauaji.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi, baada ya marehemu kukutwa akiwa amelala kitanda kimoja na mke wa mtuhumiwa,”alisema Kyando.

“Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari na kuhifadhiwa katika Hospitali ya rufani mkoani Shinyanga, ukisubili kukabidhiwa kwa wanandugu kwa ajili ya mazishi,”aliongeza.

Aidha, alisema Jeshi la Polisi mkoani humo bado linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Post a Comment

0 Comments